EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,477
- 15,325
Serikali imeanza kutafuta njia za kusafiri moja kwa moja kwenda London baada ya British Airways kusitisha huduma zake Tanzania. Mkurugenzi wa Utalii Bw. Ibrahim Mussa amesema serikali imeanza mazungumzo ya awali na Virgin Atlantic huku kukiwa na matumaini ya kufikia makubaliano na Virgin Atlantic kuchukua nafasi iliyoachwa na BA.
Amesema Septemba 2012, Virgin Atlantic ilisitisha safari zake za kwenda Nairobi baada ya miaka mitano. Amesema uamuzi wa BA kusitisha safari zake Tanzania siyo habari nzuri kwa sababu utaikosesha serikali mapato na pia ni usumbufu kwa wasafiri waliokuwa wanasafiri moja kwa moja kutoka Dar Es Salaam kwenye Heathrow.
Bw. Mussa amesema japokuwa bado haijafanyika tathmini rasmi ya madhara katika sekta ya utalii kufuatia BA kusitisha huduma zake, watalii wengi walikuwa tayari wanatumia ndege nyingine kama Emirates, Qatar and Ethiopian Airline.
Habari kutoka sekta ya usafiri wa anga zinadai kuwa BA ilikuwa moja ya ndege ambayo ilikukuwa ikisafirisha sensitive cargo kama silaha nyepesi, noti za kitaifa na kimataifa na madini kama dhahabu almasi na tanzanite kwenda soko la dunia.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Swissport Tanzania Ltd Bw. Gaudence Temu amesema kampuni yake itaathirika na uamuzi wa BA kusitisha safari zake kwa sababu imekuwa ikitoa cargo handling services tokea mwa 1985 ilipoanzsihwa.