Serikali inakosea sana inapohisi kwamba nchi ina upungufu wa walimu tu

Serikali inakosea sana inapohisi kwamba nchi ina upungufu wa walimu tu

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
2,490
Reaction score
3,584
Habari wadau!

Kiukweli serikali imekuwa ikiwapa sana kipaumbele walimu katika kuajiri pasipo kuangalia upungufu kwenye kada nyingine ambazo nazo zina umuhimu. Serikali ijitahidi kuajiri na kada nyingine kupunguza tatizo la ajira.

Ngoja niende kwenye maada kuu kiukweli nchi haina upungufu tu wa walimu bali kuna upungufu wa madawati, vifaa vya kufundishia, maabara n.k .

Na hili swala la upungufu wa walimu mashuleni serikali kamwe haiwezi kuumaliza labda kama serikali imeamua kufanya elimu ni swala la kisiasa ili kupata political mileage kupitia sera ya elimu bure.

Serikali sikivu ya rais Samia Suluhu inatakiwa irekebishe kidogo sera ya elimu bure na kuruhusu wazazi kuchangia katika elimu japo kwa udogo maana ukweli kipindi cha awamu iliyopita ilikuwa mwalimu akiomba mchango wowote inakuwa ni kesi kubwa mpaka walimu wakawa wanaogopa atakuwaambia watoto waje na hela ya uji kwa kuofia.

Lakini kwa sasa mheshimiwa anatakiwa kuongea lugha laini na wazazi na walimu kuwapa ruhusa ya kuchangisha vimichango vidogo vidogo ambavyo vinaweza kuinua elimu mfano kama kuna upungufu wa walimu katika shule basi mwalimu mkuu anaweza kuongea na afisa elimu akaita wazazi wakajadiri kuangalia kama wanaweza kuchangisha pesa kidogo kuajiri hata mwalimu wa muda the same applied kipindi cha Mzee wa Msoga hii ilisaidia walimu kuwa wengi mashuleni.

Awamu ya tano ya JPM ilikataza vimichango lakini still gap la ukosefu wa walimu wa sayansi mashuleni lilikuwa kubwa sana wapo walimu walioongea na wazazi waelewa wakakubaliana kuchangia katika elimu pia wapo walimu waliosema bora luende kwani wakifeli mimi inanihusu nini.

Serikali sasa ilegeze wazazi wasibanwe wala walimu wasibanwe kuchangia elimu kama watakaa kikao wakakubaliana.

#if you think education is expensive try.........

Mwisho nimalizie kwa kuwasalimu wote kwa jina la jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Hii ni sikivu kweli, ila kama unakuja kupima kina cha maji utakwama kweli, uli shikia kidedea elimu bure, leo unaleta hoja elimu ya kuchangia, sasa kuwa mwazi na halisi, lengo lako mi kutaka na huduma zingine ziboreshwe au watu wachangie elimu bure.
 
Hii ni sikivu kweli, ila kama unakuja kupima kina cha maji utakwama kweli, uli shikia kidedea elimu bure , leo unaleta joka elimu ya kuchangia, sasa kuwa mwazi na halisi, lengo lako mi kutaka na huduma zingine ziboreshwe au watu wachangie elimu bure.
Elimu bure lakini kuna mambo mengi hayajaboreka ktk elimu na hauwezi kungoja mpaka serikali ifanye kila kitu kwa ajiri ya mtoto wako tuache kubweteka ndio maana watoto wa International kila siku wanaongoza wao.
 
Elimu bure lakini kuna mambo mengi hayajaboreka ktk elimu na hauwezi kungoja mpaka serikali ifanye kila kitu kwa ajiri ya mtoto wako tuache kubweteka ndio maana watoto wa International kila siku wanaongoza wao.
Kweli yapo mapungufu,ila kwanini tusishauri badala ya kubeza na kukebehi. Kwa kawaidha mwathirika wa hali au mazingira anauelewa kuliko asiyeguswa na hali au mazingira. Au naseman uongo ndugu yangu.
 
Mimi nimewahi kusema kuwa walimu wa sanaa waajiriwe pia kwenye fani zingine kama utendaji wa kijiji, uafisa maendeleo na makarani wa mahakama. Hii itasaidia sana kuwaondoa hawa ndugu zetu mtaani.
 
Back
Top Bottom