KERO Serikali inaleta Ushindani kwa wazalishaji wa Ndani wa Avocado Oil dhidi ya madalali kutoka Kenya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tanzania mpaka sasahv kupitia mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya na Kagera kuna jumla ya Viwanda 12 vya kuchakata mafuta ya Parachichi

Ila serikali kupitia wizara ya kilimo na COPRA wameshindwa kuvilinda hivi viwanda na kuamua kuruhusu export ya second grade avocado kwenda Kenya kwa ajili ya kuchakata mafuta

Licha kufanya vikao na wakuu wa wilaya ya Ludewa, Wangingombe, Mbunge wa Njombe mjini pamoja na mkurugenzi mkuu wa COPRA hakuna jitihada ambazo zimeshafanywa ili kunisuru viwanda vua ndani dhidi ya ushindani kutoka Kenya.

Ikumbukwe mkenya akija anakuja kama dalali anaingia shambani na kuchuma mwenywe anafanya kulipa ushuru na kusafirisha mzigo ila wazalishaji wa ndani wanalipa kodi, SDL, PAYE kwa wafanyakazi na kutoa ajira za moja kwa moja kwa Watanzania, service levy nk

Asante naomba kuwasilisha
 
Mleta mda uchambuzi wako ni wa juu juu sana hueleweki vizuri.

Shida hapa ni nini? Viwanda vya ndani vimekosa parachichi kwa sababu zimeuzwa kwenya? Bei ja parachichi imepanda maana kenya wananunua kwa bei kubwa? Madalali wa kenya wanachuma parachichi na kuzuia wazawa wasichume? Au ishu ni nini hasa?
 
Jamaa unalalamika ila hujadadavua hasa ushindani upo wapi au unaathiri vipi hivyo viwanda vya ndani.

NACHOKIONA HAPA:
Madalali wa Kenya wananunua parachichi kwa bei kubwa kwa wakulima kuliko nyinyi wa ndani kupelekea nyie kukosa malighafi.
 
Hii tabia ya kikenge ya kulinda viwanda vya ndani wakati hata vikilindwa hamna cha maana vinafanya ndio imewatia wazazi wetu wakulima umaskini na unyonge wa kudumu na wananufaika wanasiasa na mafisadi kupitia vyama vya ushirika na mabodi yao, hii nzuri sana waache nguvu ya soko itawale vikifa potelea mbali, kwa nini wakwepe ushindani kwa kubebwa na serikali kwa expense ya wakulima maskini?, huo ni ushindani au mbeleko?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…