Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,546
- 855
Jamani Mtanzania Asitibiwe Na Serikali Yake?
Mindhali huyu shekhe mkuu ni wa BAKWATA na yuko close na wagalatia kule serikalini sitoshangaa kama kodi za wananchi zinatumika kumlipia matibabu kule India.
GT...Hii ngoma ni ya kudiscuss hapa? Wa-TZ wangapi wanatibiwa na serikali Huko India?....na sehem zingine? kaka naona unaanza kuwa LOW siku hizi. I told u ktk thread fulani hapa...Please kaa Jadili na nafsi yako na angaalia vitu sensitive !!!
Tujifunze nini ktk Hii Habari yako bro???
Kama wanamlipia Sheikh kwa nafasi yake katika dini ni suala la kujadiliwa; Si vibaya kukiwa na policy ya kuwatibia viongozi wa dini mradi iwe ni policy inayowahudumia viongozi wa dini zote na wote bila ubaguzi wala upendeleo.
Kama Sheikh mkuu anatibiwa kama mtanzania haina shida tunamtakia afya njema. Japo sijui ni vigezo gani huwa vinatumika kuamua mtanzania gani ana haki zaidi ya wengine kutibiwa nje pale matibabu ya hapa nchini yanaposhindikana.
Na kama anavuta na sigara ni vizuri pia kama mtanzania akishauriwa apunguze kuvuta sigara kwa faida yake, taifa, na wafuasi wa dini anaoaongoza.
Jamani Mtanzania Asitibiwe Na Serikali Yake?
Haya ni maoni binafsi, lakini sio ya Kitanzania (Labda wewe sio Mtanzania)
Kwa sababu Kodi inayotumika sio ya Waislam tu hapa, bali ni ya watanzania ambao wana dini mbalimbali, sasa ikisema huna neno kwasababu kodi inamuokoa Muislam mwenzi, hii sio nzuri hata kidogo, Jamii ya watanzania hatuna matatizo ya Udini, labda kama unataka kuyapandiki!!
Unadhani Kodi yako wewe(Binafsi) inaweza kumpeleka huyo Sheikh Kutibiwa India? Kama ni hapana basi jua unaitaji kodi ya Watanzania.
Na tafadhali usitake kuwa chanzo cha kuchochea mapambano katika dini zetu, please, tumia busara zako na kuwasaidia watanzania kwa ujumla na si watanzania wa dini fulani.
hiyo ya mungu kwenye nyimbo ya Taifa na kadi za krisimasi mbona hamsemi au ndio sensitive?
hiyo ya mungu kwenye nyimbo ya Taifa na kadi za krisimasi mbona hamsemi au ndio sensitive?