JosepCosta1258
New Member
- Oct 7, 2026
- 1
- 1
Suala la Kanzidata kwenye mfumo wa ajira Tanzania ni mtambuka. Serikali inapaswa kueleza uhaba wa nafasi kwenye taasisi za umma unatokana na nini, ilhali zinatoa nafasi za ajira za mkataba kwa kada hizohizo zilizopo kwenye Kanzidata.
Kigezo kinatajwa kuwa taasisi haina uwezo wa kulipa mishahara, ilhali kuna upotevu mkubwa wa fedha na matumizi holela ambayo yanaweza kutumika kupunguza ombwe la uhaba wa ajira.
Mfano, wizara kama Elimu, Kilimo na Maliasili, ambazo ni uti wa uchumi, bado serikali haioni haja ya kuingiza vijana? Wizara ya Maliasili na Utalii, leo ni 2026, lakini bado inatumia sera ya 1999 na mipango ya miaka hiyo.
Vijana wananyimwa nafasi na kutakiwa kujitolea, na mkataba ukiisha unarudi nyumbani kwenu kulima. Au serikali inachuki na vijana?