Serikali inapaswa kuwaeleza Wananchi kuwa watanufaikaje na huu uwekezaji wa DP World

Serikali inapaswa kuwaeleza Wananchi kuwa watanufaikaje na huu uwekezaji wa DP World

Je, unafahamu faida za uwekezaji wa DP World?

  • Ndio

    Votes: 0 0.0%
  • Hapana

    Votes: 1 100.0%
  • Sina uhakika

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    1

Mr Why

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2019
Posts
2,235
Reaction score
4,252
Mengi yanazungumzwa sana kuhusiana na mkataba wa DP World huku maswali mengi yakikosa majibu. Watanzania wanaonesha kutoridhika na uwekezaji wa DP World katika bandari za Tanzania kwa kutokuridhishwa na majibu ya maswali yao. Watanzania wanasema kuwa hawapingi uwekezaji wao wanataka kufahamu matunda yake.

Maswali mawili muhimu yanayozunguka akilini mwa watu kila uchwao pasipo na majibu ni kuwa

Kikomo cha mkataba huu ni kipi?
(Ikumbukwe kuwa kikomo cha mkataba wowote ule ni cha kuzingatia sana kwasababu uwekezaji unaweza kufanya makosa ikiwa hakuna kikomo basi Watanzania watabeba matatizo yasiyo na kikomo)

Je, Watanzania watanufaikaje na huu mkataba?

Watanzania wengi wamekata tamaa, na ili imani irudi basi Serikali inashauriwa kuwajibu Wananchi maswali haya makubwa mawili.
 
Watanzania acheni uvivu na kulishwa matango poli.

Ule mkataba upo tulia na usome.

"Ukitaka kumficha mwafrika weka ujumbe kwenye vitabu"

Ujinga.
 
Watanzania acheni uvivu na kulishwa matango poli.

Ule mkataba upo tulia na usome.

"Ukitaka kumficha mwafrika weka ujumbe kwenye vitabu"

Ujinga.
Wapo watu wenye matatizo ya macho kwahiyo kuna haja ya kuzungumza hadharani hili sio swala la faragha
 
Back
Top Bottom