Serikali imependekeza hatua kadhaa za kodi kwa mwaka wa fedha 2026/27 ili kuchochea matumizi ya nishati ya umeme na gesi asilia nchini.
Hatua hizo ni pamoja na kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye vifaa vya vituo vya kuchaji magari ya umeme vinavyoingizwa nchini, kupunguza ushuru wa forodha wa magari ya umeme kutoka asilimia 25 hadi 10, pamoja na kuendelea na mazungumzo na viwanda vya kuunganisha magari nchini kuhusu utoaji wa unafuu wa kodi kwa waunganisha magari ya umeme.

- Mosi, kusamehe kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye vifaa vitakavyotumika katika vituo vya kuchaji magari yanayotumia umeme vinavyoingizwa nchini vinavyotambulika kwa HS 850400.
- Pili, kupunguza ushuru wa forodha kutoka 25% hadi 10% kwenye magari yanayotumia nishati ya umeme yanayotambulika kwa HS codes ambazo zimeonyeshwa katika hotuba yangu. Aidha, serikali inaendelea kufanya majadiliano na viwanda vya kuunganisha magari vilivyopo nchini ili kutoa unafuu wa kodi kwa waunganisha wa magari ya umeme hapa nchini.
- Na tatu, kusamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye mita janja za gesi ya mitungi ya kupikia (yaani LPG smart meters) zinazoingizwa nchini zinazotambulika kwa HSC 9028.10.00; msamaha husika utatolewa kwa wasambazaji wa gesi ya kupikia pekee.