Blesscountry
New Member
- May 29, 2024
- 2
- 4
Habari za muda huu Rais Samia, nakupongeza kwa uongozi wako kama Mama wa Taifa letu, huku ukidumisha nafasi yako kama Rais.
Rais Samia, mimi ni mmoja wa vijana wachache tuliojiajiri na tunachangia pato kubwa kwa Taifa letu la Tanzania. Hivi sasa tunakutana na changamoto kubwa sana. Mheshimiwa Waziri amefungia Ziwa Tanganyika kwa miezi mitatu kutokana na upungufu wa samaki aina ya Migebuka na Dagaa, na mimi kama mwananchi naunga mkono hatua hiyo.
Hata hivyo, kuna changamoto ambayo Mheshimiwa Waziri hakuizingatia. Ziwa Tanganyika halitoi tu samaki wa chakula, bali pia linatoa samaki wa mapambo, ambao ni biashara ya Watanzania wengi na kuna makampuni zaidi ya mia moja nchini.
Rais Samia, kutufungia sisi wavuvi wa samaki wa mapambo kwa miezi mitatu ni kutusababishia hasara kubwa. Tutashindwa kuhuisha leseni zetu kutokana na gharama kubwa za leseni, ambazo zimepanda hadi milioni 10 kwa mwaka. Aidha, kipindi cha mvua na upepo kinapoanza kuanzia Desemba hadi Machi, hatuwezi kufanya kazi kwa sababu maji yanakuwa machafu na samaki hawaonekani.
Pili, Serikali yetu imefunga tena Ziwa Tanganyika kwa miezi mitatu kuanzia Mei hadi Agosti, na hii pia ni changamoto kwetu kwani kuanzia Agosti nchi nyingi hazichukui mzigo wetu kwa sababu ya hali ya baridi. Hii itasababisha makampuni mengi kufilisika, hasa yale yanayouza samaki Ulaya.
Rais, sasa hivi wafanyabiashara wa samaki wa mapambo tupo kwenye wakati mgumu sana. Serikali yetu imefunga ziwa kwa ajili ya samaki wa chakula tu, lakini haijazingatia biashara yetu ya samaki hai. Waziri hajatoa sababu yoyote inayotufanya sisi tusifanye kazi, bali maafisa wa uvuvi wanatuzuia kwa sababu wanahofia wavuvi wengine watahoji kwa nini sisi tunaruhusiwa kuvua.
Rais, tunaomba msaada wako kwani hali yetu ni mbaya sana. Wako Mtanzania mtiifu na mlipa kodi. Asante Mama yetu, matumaini yetu ni juu yako kama ulivyoweza kutatua changamoto zingine, pia tuna imani hii utalimaliza. Asante.
PIA SOMA
- UPDATE: Serikali yaahirisha kufungwa kwa Ziwa Tanganyika