A
Anonymous
Guest
Kumekuwa na utaratibu wa kikodi wa kiholela sana unaocha mianya ya rushwa ya wazi kabisa kwa Ofisi ya Madini hasa kwa eneo nililolitaja, nadhani utaratibu huu unatumika kote nchini, hapa wilaya ya Tarime, Mkoa wa Mara.
Mwishoni nitatoa pendekezo langu juu ya nini kifanyike namna nzuri ya kukusanya haya mapato ili yasiishie mikononi mwa watu wachache waliopewa dhamana ya kusimamia sekta hii.
Sijataka kupresent hii kwa ID yangu ingawa mimi ni mkongwe humu, najua hii inaenda kuharibu kula ya baadhi ya wanene.
Iko hivi, Uko utaratibu umewekwa na Ofisi ya Madini mkoa, kila mmiliki wa kremu (active) cha uchimbaji madini, mbali na kodi anayokatwa anakoenda kuuza dhahabu yake Sokoni (ingawa ukweli dhahabu inayouzwa sokoni ni almost 40-50% ya dhahabu yote! Nna uhakika na hili! Nyingi haipiti sokoni kabisa!) kuna kodi nyingine (hii ndiyo ninayoiangazia hapa)...
Mmiliki wa kremu cha uchimbaji huwa anahodhi maeneo ya kuchimba dhahabu kwa watu binafsi wenye uwezo kifedha ili wafungue mashimo kwenye kremu chake (anachokilipia yeye mwenyewe mmiliki leseni), Watu hawa wanaweza kuunganisha nguvu kifedha wakawa hata 10 kuanzisha shimo 1, maana uchimbaji ni gharama...
Hivyo basi, kremu kimoja kinaweza kuwa na mashimo ya watu tofauti hata 50 (mashimo 50, wamiliki tofauti) kulingana na ukubwa wa eneo la kremu chake anachokilipia kihalali.
Twende taratibu utanielewa tu...
Sasa iko hivi... Kwa mfano, Mimi Ninaweza kuwa na ardhi, naimiliki kihalali kabisa na document nnazo, lakini mwenye leseni ya uchimbaji wa madini yaliyoko chini ya ardhi yangu ni mtu mwingine tofauti! (Hivi ndivyo ilivyo!)
Hapa ndipo ukaibuka utaratibu wa kodi wa asilimia 30 yaani 10/3 ama 10 kwa 3... ambayo sasa sio 10 kwa 3 tena! Bali ni 10 KWA 4...!
Huu ni utaratibu uliwekwa baada ya marehemu Mwenda zake kuingia madarakani... ndipo utaratibu huu ulianza kazi rasmi.
NA WATU WA OFISI YA MADINI KUWEKA KAMBI RASMI KWENYE ENEO LOLOTE LENYE UCHIMBAJI HAI (unaofanyika)
Nifafanue kidogo hapa....
Kwamfano... Mimi ni mmiliki wa shimo, nikitoa viroba 100 kwenye shimo langu, Viroba vyangu (Taxed) vitakuwa ni viroba 60 na viroba 40 vinavyobaki vinaenda kwenye huo mgawanyo hapo juu! (hivi ni viroba vya mawe ya leaf (dhahabu gredi ya juu inayoonekana kwenye jiwe kwa nacho) ambayo inakamatwa kwa kuoshwa na zebaki (mercury).
Na pia ipo dhahabu isiyoonekana kwa macho (hii inaitwa fero) ambayo hupelekwa mwaloni kusagwa, kupigwa mtambo na baadaye kupelekwa plant kukamatishwa na madawa ya kikemia kama Cynide, n.k kisha kumalizika kwa carbon iliyokamata dhahabu toka plant kwenda kuchomwa illusion plant na kupatikana Pure gold.
Katika kila mgawanyo wa madini haya ghafi pia ama fero ama casually naweza kuyaita makinikia, mgawanyo wake huwa ni huo huo 10/4 hapa mwenye shimo akitoa fuso kumi za mawe, fuso 4 zinaenda kwa mwenye kremu, ardhi na ofisi ya madini.
Hapa kwenye huu mgawanyo ndipo imeachwa mianya ya wazi ya rushwa! Maana Ofisi ya Madini huwa wapo kila siku na ina ratiba ya kila shimo ni lini inatoa fero ama viroba vya lifu.
Sasa basi shimo fulani linapokuwa linasomba siku hiyo... kama wamekadiria mzigo uliopo ni fuso 100... wanaanza kwa kutoa kwanza hizi fuso zao 40 then zinazobaki anaruhusiwa sasa mwenye shimo kusomba kupeleka atakako (kwenye mwalo wake ama kuuza kama ataamua).
Sasa basi kwenye huu mgao wa madini wa asilimia 1 yaani fuso 10/100 HIZI FUSO ZA MAWE ASILIMIA MOJA WANAZOPEWA OFISI YA MADINI... HUWA WANAZIUZA PALEPALE! SHIMONI KWA MAKOTA! Tena kwa bei ya chini tofauti na wengine wanavyouza! Na wana matajiri wao spesho!
Kwa muktadha huu, hii hela huwa inaishia mifukoni! Tunaona, tunajua, na tuna uhakika! Maana ni watu tuko nao mtaani, baani, makanisani, misikitini, kwenye sherehe tunajumuika nao!
Sasa Basi Ningependekeza kupendekeza yafuatayo...
Serikali iratibu utaratibu utakaohusisha maofisa wa kodi, mmiliki wa kremu mmiliki wa shimo KUWEKA UTARATIBU WA KUILIPIA TOZO HII YA 1 PERCENT KWA KUTUMIA CONTROL NUMBER, KILA SHIMO LISAJILIWE NA KUPEWA CONTROL NUMBER YAKE TOFAUTI.
Na uratibu huu ufanywe chini ya TRA maana hawa Maofisa Madini kwa wenye vilemu na mashimo wanawamudu! Ni maswahiba.
NB: Angalizo:
Bei ya Fuso moja ya fero (madini ya dhahabu ghafi ni 2,500,000-4,000,000/=( kwa eneo nililolitaja)
Kiroba kimoja cha lifu ni Tsh 600,000-3,000,000/=
Hii hutegemeana na sempo ilivyo, kuna wakati bei inaweza kupanda zaidi ya hapo! Ama kushuka chini pia zaidi ya hapo! Hivyo bei hizi huwa sio constant.
Nawasilisha.
Pia soma ~ Maisha ya watu wa Nyamongo yanazidi kuwa tete