Serikali inawachelewesha bodaboda, ni mabomu mtawanyiko yanayotembea

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Wazungu wana msemo wao usemao adui yako mkabidhi pikipiki.
Wakiwa na maana kwamba pikipiki ni usafiri hatari sana kwa maisha, haupaswi kuutumia kila siku kutwa nzima.

Tanzania bado fursa salama kuliko bodaboda kwa vijana ni nyingi sana kama serikali ikiamua kuzimulika vijana wazione.

Hasara wanazopata bodaboda na wanazosababisha kwa wengine na taifa ni kubwa kuliko kama watu wanavyodhani. Wanaumia na kufa wengi, wanaharibu magari ya wengine barabarani, wanaharibu barabara ili wapate sehemu za kuvukia kwa urahisi, wanaiba na kufanya uhalifu kwa kutumia bodaboda, wanagonga watoto na watu mitaani.

Tanzania bado ina nafasi kwenye kilimo, ufugaji, uvuvi, uchimbaji, biashara, viwandani, sanaa, michezo na ajira. Tufanye kila kitu tuwaondoe vijana hawa barabarani kwa kuwaonyesha fursa nyingine salama zaidi kwao.

Bodaboda hizi pia zinawasababishia magonjwa ya njia ya hewa, uhanithi, uchovu na msongo wa akili. Wengi wanakabiliana na halii hii kwa kuvuta bangi, kunywa pombe na vinywani vya energy.

Bodaboda ni rahisi sana kutumiwa kwa malipo na watu waovu kujipatia kipato.

Mbaya zaidi kwa wanasiasa wamepunguza adhabu ya makosa kwa bodaboda kutoka 30,000 hadi 10,000. Hii inaongeza idadi ya makosa kwa bodaboda.

Serikali chakavu itawahesabu bodaboda kama watu wenye ajira.
 
Uko sahihi sana!
Hongera kwa mtazamo mzuri mpana!! Japo najua ni ngumu sana kufanyiwa kazi hayo mawazo yako kwa sababu wafanya maamuzi wanawatumia hao bodaboda kwa faida zao pia.
 
Mneshawatumia wakati wa uchaguzi sasa hivi mnaona tatizo.
Kama wakati wa kampeni mliwagawia pikipiki tatizo ni hao think tank wenu.
Pikipiki na baiskeli walizopewa zilitumika tu kuhimiza wapiga kura waende kupiga kura asubuhi na mapema kabla wengine hawajaamka. Ndio maana CCM wote walimaliza kupiga kura kabla ya saa 5 asubuhi. Hazitumiki kama bodaboda zile.

Hata hivyo usafiri wa bodaboda serikali isiuhesabu kama ajira ya vijana, ni mateso kwa vijana na hasara kwa wengine na taifa. Vijana wote hawa wenye bodaboda wanaweza kumezwa na kilimo, uvuvi, ufugaji na biashara. Na wachache wakamezwa na utumishi wa umma na private na uchimbaji.
 
hili la kugonga watoto na watu mitaani, nimeapa nitachinja watu, kwanzia dereva mpaka na familia yake,kama sina akili nzuri,..... habari za kwamba mtu agonge mtoto wangu, alafu aje na tupesa twake eti kuniomba samahan,......
itakuja kuweka kichwa kikubwa sana cha habari hapa nchini,....
acha mtu ajichanganye
 
chadema ikikamata madaraka kitu cha kwanza itapiga marufuku bodaboda wote na kusitisha uingizaji wa pikipiki nchini
 
Uko sahihi sana!
Hongera kwa mtazamo mzuri mpana!! Japo najua ni ngumu sana kufanyiwa kazi hayo mawazo yako kwa sababu wafanya maamuzi wanawatumia hao bodaboda kwa faida zao pia.
Hata kama hawataki lakini bodaboda ndio adui yao namba moja CCM na serikali yake. Bodaboda hawa hawakatai kazi yoyote yenye malipo kwao bila kujali matokeo yake.

Mashariti ya kuendesha pikipiki lazima yawe magumu sana ili kuwasukuma vijana kwenye kazi nyingine salama kwao.
 
chadema ikikamata madaraka kitu cha kwanza itapiga marufuku bodaboda wote na kusitisha uingizaji wa pikipiki nchini
kwahiyo unafuta ajira mchongo yenye watu zaidi ya Milioni 1.5,,, halafu huna solution ya haraka?...
 
Pikipiki na baiskeli walizopewa zilitumika tu kuhimiza wapiga kura waende kupiga kura asubuhi na mapema kabla wengine hawajaamka. Ndio maana CCM wote walimaliza kupiga kura kabla ya saa 5 asubuhi. Hazitumiki kama bodaboda zile.

Hata hivyo usafiri wa bodaboda serikali isiuhesabu kama ajira ya vijana, ni mateso kwa vijana na hasara kwa wengine na taifa. Vijana wote hawa wenye bodaboda wanaweza kumezwa na kilimo, uvuvi, ufugaji na biashara. Na wachache wakamezwa na utumishi wa umma na private na uchimbaji.
Bodaboda ni ajira, acha kuwaonea wivu.
 
You can't be serious kuna pahala ni kama unesema uhanithi sijui
 
Tulipofikia sijajua wanaziondoaje!

Uwe mpango wa miaka 20,hakuna kuingiza pikipiki wala spares zake mpaka zilizopo ziishe.

Wakulima,Wavuvi,Wafugaji,Wachimbaji na Waajiriwa side hustle ni kuendesha bodaboda kwa sasa.

NB:CCM wala haihitaji kura za bodaboda kushinda uchaguzi.
 
Bodaboda ni ajira, acha kuwaonea wivu.
vilema na vifo ni vingi sana huko vijijini. Tumeshapoteza mjukuu kagongwa na bodaboda akicheza, tumepoteza mfanyabiashara mdogo anatoka kufungasha bidhaa za kiduka chake, bodaboda zinagongana na kugonga. Watu hawana ujuzi wa barabara kabisa lakini wanaendesha barabarani sawa na magari.

Magari yangu yana makovu kila kona ya kukwaruzwa na bodaboda, taa na saiti mirrors nimenunua sasa nimeacha tu na kreki zake. Anakugonga na kukimbia. Hasara ni kubwa sana aloo. Watu wanaibiwa
 
Wazungu wana msemo wao usemao adui yako mkabidhi pikipiki.
Wakiwa na maana kwamba pikipiki ni usafiri hatari sana kwa maisha, haupaswi kuutumia kila siku kutwa nzima.

Tanzania bado fursa salama kuliko bodaboda kwa vijana ni nyingi sana kama serikali ikiamua kuzimulika vijana wazione.

Hasara wanazopata bodaboda na wanazosababisha kwa wengine na taifa ni kubwa kuliko kama watu wanavyodhani. Wanaumia na kufa wengi, wanaharibu magari ya wengine barabarani, wanaharibu barabara ili wapate sehemu za kuvukia kwa urahisi, wanaiba na kufanya uhalifu kwa kutumia bodaboda, wanagonga watoto na watu mitaani.

Tanzania bado ina nafasi kwenye kilimo, ufugaji, uvuvi, uchimbaji, biashara, viwandani, sanaa, michezo na ajira. Tufanye kila kitu tuwaondoe vijana hawa barabarani kwa kuwaonyesha fursa nyingine salama zaidi kwao.

Bodaboda hizi pia zinawasababishia magonjwa ya njia ya hewa, uhanithi, uchovu na msongo wa akili. Wengi wanakabiliana na halii hii kwa kuvuta bangi, kunywa pombe na vinywani vya energy.

Bodaboda ni rahisi sana kutumiwa kwa malipo na watu waovu kujipatia kipato.

Mbaya zaidi kwa wanasiasa wamepunguza adhabu ya makosa kwa bodaboda kutoka 30,000 hadi 10,000. Hii inaongeza idadi ya makosa kwa bodaboda.

Serikali chakavu itawahesabu bodaboda kama watu wenye ajira.
Hao ndiyo mtaji wa viongozi wetu, hukumbuki pikipiki zenye mchanganyiko wa rangi za timu ya mpira maarufu
 
Back
Top Bottom