Serikali inawachukulia hatua gani waajiri wanaoipatishia hasara serikali kwa kufukuza kazi watumishi kihuni?

Serikali inawachukulia hatua gani waajiri wanaoipatishia hasara serikali kwa kufukuza kazi watumishi kihuni?

Konseli Mkuu Andrew

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2013
Posts
749
Reaction score
875
Kumezuka tabia ya watumishi wa umma kufukuzwa kazi kihuni na waajiri wao na kutokana na kutofuraishwa na kufukuzwa kwao , watumishi hao huwa wanaenda kufungua malalamiko huko CMA Commission for Mediation and Arbitration na mwishowe huwa maamuzi hufikiwa idara hiyo ya serikali hutakiwa kumlipa fidia huyo mwajiriwa.Je serikali imeweka mkakati gani juu ya hawa waajiri ambao hufukuza watumishi kihuni pasina kufuata utaratibu wa kisheria? Isije kuwa tunalalamika serikali inapoteza pesa kila mwaka kumbe huwa zinapoteza kwa style hii.

Huko kwenye mashirika binafsi hii mbinu hutumiwa sana na mwajiriwa na baadhi ya wenye vyeo kwenye kampuni kumfukuza kazi mwajiriwa kihuni na baadae hizo fidia wanakuja kugawana.Waswahili wanasema kila mbuzi hatakula kulingana na urefu wa kamba yake.

Nitaleta baadhi ya kesi zilizofikiwa maamuzi na mahakama au tume ya usuluhishi zinazohusiana na masuala ya waajiri kuwafukuza watumishi kihuni na kuipatishia hasara idara husika.


Mnadhimu Mkuu
 
Chadema Mwacheni Mama Apumue..!
Punguza kukariri jombaaa.Sometimes itanue akili kwa kudiscuss mambo yenye tija kwa taifa lako, huo ndo uzalendo na sio kusema mi5 tena.Au hutaki kukumbukwa na vizazi vijavyo kwa mema? Shauri yako jombaaa.Usije sema sikukwambia.
 
Back
Top Bottom