Serikali inayapangia Magazeti kitu cha kuandika? Tazama haya magazeti

Serikali inayapangia Magazeti kitu cha kuandika? Tazama haya magazeti

Gulwa

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2008
Posts
10,597
Reaction score
16,394
Leo nimeshtushwa na magazeti haya mawili katika kurasa zao za mbele kubwa na vichwa vya habari vinavyofanana.

b9211235-2bcc-4892-a506-41edb45a7e09.jpeg

be5adb18-7812-48dc-8c69-e577ecaed782.jpeg


Kumekuwepo na tetesi kwamba serikali imekuwa ikiyapangia magazeti habari za kuandika.

Kati ya magazeti ambayo yalikuwa yamebaki na uhuru kidogo ni haya ya Mwananchi Communication, sasa nayo yamemezwa.

9349d741-029a-4ee9-b22b-1ef30716fb49.jpeg

943c8644-5883-49e4-9d8a-0ccf858ea0c7.jpeg


Tuzidi kutafuta pesa za kununua MB za kutosha tuweze kujitafutia habari mitandaoni.
 
Ni vizuri ungeweka kabisa kapicha ka kuonyesha content za kufanana kwenye hayo magazeti hapa.

Yote kwa yote, Samia na Chawa wake wameiga mtindo ule ule wa Magufuli kuvifanya vyombo vya habari visiwe huru, Magufuli alikuwa anatumia nguvu ya moja kwa moja (vitisho vya kupotezwa) na Samia anatumia nguvu ya nyuma ya pazia (hongo na misamaha ya kodi).

Wameshindwa tu kwenye mitandao ya kijamii hususani JF.
 
Media zote Tanzania zipo blackmailed

Tena hao mwananchi ndio inamilikiwa na kina February sasahivi
 
Jambo la ajabu sana hili, Bajeti imesomwa jana, ila Magazeti makubwa yote yameamka na Kichwa cha Habari kimoja. Hii ni ushahidi tosha kuwa ni maelekezo kutoka Mamlakani au Takrima kwa Wahariri ili waandike kile Serikali inataka kukiona.

Angalia hapa
1686899942234.png

1686900009703.png

1686900022744.png

1686900035468.png
 
Mbona ni hesabu rahisi sana

Chukulia we unaweza kupiga bilioni 300 Kila mwaka kupitia ufisadi kutokana na nafasi uliyonayo, ili kutoipoteza Hio nafasi unatenga budget ya let's say bilioni hata 50 kuhonga watu wapige propaganda na kukusifia uendelee kuwepo kwa huo wadhifa, unabaki na 250 bilion

Mwaka ujao unatumia tena same strategy!! Mbona ni biashara rahisi sana
 
Media zingine wao wanaambiwa wazungumzie mipira,betting,miziki na masingeli+udaku

Ova
 
Back
Top Bottom