Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 26,483
- 40,130
Wanabodi poleni kwa majukumu ya kufukuzana na shilingi inayopepea.
Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kisasema 'Kila mtu anayo Haki ya kuishi na kupata kutoka katika jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria' mwisho wa kunukuu.
Dunia sasa hivi inapitia wakati mgumu sana kutokana na janga la mlipuko wa maambukizi ya COVID-19 ambayo yaligunduliwa awali katika jimbo la Wuhan nhini China. Nchi zote duniani ni wahanga wa hili janga ambalo limesababisha madhara makubwa kwa uhai wa binadamu kwa kipindi kifupi sana.
Wimbi la kwanza la mlipuko huu tulishuhudia athari kubwa za huu ugonjwa ambapo sisi kama taifa tulipoteza wapendwa wetu wengi sana. na sasa wimbi la pili limekuja huku kukiwa na juhudi zilizozaa chanjo ambayo inaweza kuwa ni mwarobaini wa janga hili.
Kwa kuzingatia Ibara ya 14 ya katiba yetu,
Wanasheria mpo na mmekaa kimya kwenye hili hivyo historia itatuhukumu wote bila kubagua yaani sisi ytuliopiga kura kishabiki na nyie wenye uwezo wa kuchukua hatua za kikatiba na sheria lakini mkakaa kimya.
Serikali zingatieni haki ya kila Mtanzania hasa Haki ya kuishi kwa kutoa taarifa (zisizo za taharuki) sahihi kuhusiana na hii hali inayoendelea. pia izingatie haki ya wanaopenda kupata chanjo ya Corona wapatiwe na sisi wenye nyungulization tuendeleze libeneke bila bughudha.
Uzi

- Je serikali yetu imetimiza wajibu wake kutuhakikishia haki ya kuishi?
- Watanzania wengi tumehamasishwa kutumia njia za asili kujikinga na kutibu dalili zake, je wale wachache wanaohitaji chanjo wamezingatiwa haki yao ya kuishi?
- serikali kupitia Rais kukanusha uwepo wa CORONA nchini kumezingatia haki ya Ibara ya 18 (d) "Kila mtu anayo Haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii" mwisho wa kunukuu. Hali hii ya watu wengi wanaokufa na hata huko hospitalini kujaa wagonjwa wenye shida ya kupumua ambapo wengi huishia kupoteza uhai wao, je serikali imezingatia haki ya kuishi kwa watu wake?