Serikali inazingua lakini na sisi tunajisahau mno

Serikali inazingua lakini na sisi tunajisahau mno

nguvu ya buku

Senior Member
Joined
Jul 15, 2025
Posts
168
Reaction score
549
Watu wengi wakipata nafasi, wanaangalia zaidi namna ya kuinua familia / ndugu zao, si kwa maslahi ya taifa au jamii kwa ujumla.

Mradi mtu na familia / ndugu wake wako vizuri, basi huhisi nchi haina shida hata kama jirani anaumia, hata kama mfumo mzima unaporomoka, wao hayawahusu.

Hiki ndio chanzo kikuu cha uchawa na pengo kubwa la utofauti wa kipato. Tumekuwa taifa la "mimi na wangu", badala ya "sisi pamoja".

Kama hatutabadilika na kujenga fikra za pamoja, tutaendelea kuishi kwenye mzunguko wa ubinafsi, ukimya, na umasikini wa kifikra.

Utaifa haujengwi na serikali peke yake, unajengwa na raia wenye moyo wa pamoja.
 
Someni katiba muielewe then mtaweza kuwajibisha serikali.
 
Back
Top Bottom