Serikali ingefanya haya kama mbadala kuwatua wananchi mzigo wa tozo
- Kuweka usimamizi mzuri wa fedha za umma, kuhakikisha fedha zote zitokanazo na ushuru, madini, utalii na kodi mbalimbali zinaingia mahali stahiki.
- Kupunguza matumizi na gharama zisizo za lazima kama kununua magari ya gharama kubwa, safari zisizo za lazima kwa viongozi, na kupunguza misururu ya misafara ya viongozi.
- Kuondoa/kupunguza tozo na kodi kwenye bidhaa muhimu kama vile mafuta.
- Pia serikali ione haja ya kuwekeza kwenye kilimo na ufugaji moja kwa moja badala ya kuingiza siasa, hii itapunguza uhitaji wa uagizaji bidhaa za vyakula kutoka nje na itaongeza mapato kwa mauzo ya bidhaa za kilimo nje ya nchi.