DOKEZO Serikali ingilieni kati Fidia ya Uharibifu wa Mazao yaliyoharibiwa na Tembo Wilayani Ngara - Kagera: Sheria ya Wanyamapori inakandamiza Wakulima

DOKEZO Serikali ingilieni kati Fidia ya Uharibifu wa Mazao yaliyoharibiwa na Tembo Wilayani Ngara - Kagera: Sheria ya Wanyamapori inakandamiza Wakulima

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Ikiwa ni siku chache tu tangu Kundi la Tembo kutoka Hifadhi ya Burigi - Chato kuvamia Mashamba na Makazi ya Wakulima wa Kata ya Kasulo, Wilayani Ngara Mkoani Kagera, Wananchi wengi walioathirika na uvamizi huo wamepoteza matumaini yao huku wakijiandaa kukabiliwa na balaa la njaa kwa mwaka huu.

Licha ya Tembo hao kusababisha Kifo cha Mwanamke mmoja pia bado mashamba mengi za Wakulima yameharibiwa huku mazao yakiwa katika hatua za mwisho mwisho katika ukomavu.

Fidia zilizoainishwa na Maafisa wa TANAPA kutoka kwenye Sheria ya Wanyamapori siyo stahiki kwa Wananchi kwasababu fidia hizo zimejikita sana kwenye umbali toka eneo la hifadhi na siyo aina ya mazao au tathmini ya uharibifu alioupata mkulima.

Licha ya kuwa Mashamba yaliyovamiwa yapo zaidi ya 20Kms kutoka mpaka wa Hifadhi lakini sisi kama Wananchi tungeiomba Kamati ya Maafa ya Wilaya, Mkoa na Taifa (kupitia Wakala wa Taifa wa Uhifadhi wa Chakula - NFRA) kufika kwa upesi kufanya tathmini nyingine ili kuona ni namna gani wanaweza wakainusuru Wilaya ya Ngara kwa njaa ya Mwaka huu pamoja na Familia zote zilizoathirika.

IMG-20250209-WA0059.jpg

IMG-20250209-WA0057.jpg
IMG-20250209-WA0061.jpg
IMG-20250209-WA0067.jpg
IMG-20250209-WA0068.jpg

Pia soma ~ Rais Samia: Viwango vya Fidia kwa wanaoathiriwa na uvamizi wa Wanyama viangaliwe
 
Back
Top Bottom