Jambo hili tulitaadhalishwa na mwanasiasa na mwanasheria hasiyependa unafiki na msema kweli daima, Tundu Lissu. Lakini vichwa vya vyetu vilishageuzwa kushabikia ujinga unaofanya na Serikali, tulimuona na kumuita Lisu majina ya ovyo ya kila aina na zaidi kumpa zawadi ya marisasi.Kwamba mikataba ya kipuuzi iliyoingiwa kwa rushwa na ubinafsi wa watu wachache sio shida?
Root cause ya hizo fidia na mikesi yote ni nini kama sio hiyo mikataba ya hovyo.
Labda ungesema (tulishakosea nyuma kama taifa kuingia mikataba ya kimangungo, hatuna budi kuwa wapole kuendana na hali halisi, cha kuzingatia madhara yasiwe makubwa kwa taifa) ila kamwe usiseme shida sio mikataba kuingiwa kinajisi.
ingekua sio shida wala hamna mtu angeandika habari za mikataba wala fidia.
Mikataba mibovu imekuwa iliingiwa kibabe na serikali ya CCM, ikipigiwa kelele sana hasa na vyama vya upinzani. Mwendazake yeye kaja kuivunja kijingakijinga. Tunatafunika na tutaendelea kutafunika. Sioni haja ya kuwa na ofisi ya mwanasheria mkuu, kama kila wakati wanalidhia na kupitisha mambo ya hovyo yanayofanywa na wanasiasa. Kwa kinachoendelea ni kama hatuna wanasheria nchini!!