Serikali iondoe kesi zote ICSID na kutafuta namna ya kulipa fidia

Jambo hili tulitaadhalishwa na mwanasiasa na mwanasheria hasiyependa unafiki na msema kweli daima, Tundu Lissu. Lakini vichwa vya vyetu vilishageuzwa kushabikia ujinga unaofanya na Serikali, tulimuona na kumuita Lisu majina ya ovyo ya kila aina na zaidi kumpa zawadi ya marisasi.

Mikataba mibovu imekuwa iliingiwa kibabe na serikali ya CCM, ikipigiwa kelele sana hasa na vyama vya upinzani. Mwendazake yeye kaja kuivunja kijingakijinga. Tunatafunika na tutaendelea kutafunika. Sioni haja ya kuwa na ofisi ya mwanasheria mkuu, kama kila wakati wanalidhia na kupitisha mambo ya hovyo yanayofanywa na wanasiasa. Kwa kinachoendelea ni kama hatuna wanasheria nchini!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…