Serikali iondoe Kodi kwenye uingizaji wa mashine za uzalishaji, ili kupunguza tatizo la ajira

Serikali iondoe Kodi kwenye uingizaji wa mashine za uzalishaji, ili kupunguza tatizo la ajira

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Vijana wengi wapo idle hawana kazi wana bet tu
Naomba serikali iondoe Kodi kwenye uingizaji wa mashine za uzalishaji

Vile vile Kuna ukiritimba wa uagizaji hasa wa zana za kilimo na pembejeo, Kuna matajiri wanapata vikwazo wakitaka kuagiza, maana Kuna viongozi wa serikali ndo wana hiyo nafasi ya kuagiza na kuuza bei kubwa Kwa wakulima

Mfano China tractor ni million 3 ila kufika huku litauzwa million 10
Tractors zikiwa cheap ni rahisi kuwashawishi vijana kulima, Sasa ni ngumu kumshawishi kijana kutumia jembe la mkono

Mashine zingine kama za kufyatua matofali, kuoaka mikate, kupasua mawe, mashine za kutotolesha vifaranga n.k zikipatina Kwa unafuu wa bei zitawafanya vijana wajiajiri kirahisi

Serikali imeondoa Kodi kwenye taasisi za dini, yaani Leo askofu anaweza kuingiza magari ya kifahari 200 Bure ila kuingiza tractors ni Kodi kubwa mno ambayo unasababisha upatikanaji kuwa mgumu

Serikali ufikirie vijana na kuhakikisha hasa zana na pembejeo za kilimo zinapatikana kirahisi
 
Kwani hujui hizo taasisi za dini na serikali ni watoto wa baba mmoja wanaotumia mbinu tofauti kumyonya binadamu hapa duniani?
If you can't beat then join them.
 
Mashine zinategemea ukubwa wa uzalishaji, kwa mashine za viwanda vidogo zitengenezwe hapahapa nchini
SIDO wapewe ruzuku wazalishe mashine nyingi na kupatiwa raia kwa mkopo
VETA nao wapewe ruzuku ktk utafiti na uundaji wa vifaa vya kisasa
 
Serikali iliangalie hili.

Ikiwezekana wale wanaoanza kujiajiri/biashara wasilipe Kodi ya Serikali wa miezi 6 au Mwaka 1 ili waweze kua na nafasi nzuri ya kupiga hatua.
 
Serikali haijali kuhusu mwananchi wa kawaida,ndiyo maana tunakamuliwa kodi kuanzia mwanzo kabisa wa biashara.
 
Serikali ipunguze bei ya viwanja vya kujengea viwanda, viwanja vya kuweka biashara. Kuuza kiwanja cha kiwanda kwa @20,000 kwa mita moja ya mraba au 30,000 kwa sqm au 50,000 kwa sqm ni bei juu mno na inaua uzalishaji wa bidhaa hasa kwa vijana na wazawa, hakuna kijana mwenye milioni 500 au 1B kwa ajili ya kununua kiwanja cha kiwanda. Hapo kwa bei hiyo labda anunue mtu tajiri sana au mwekezaji toka china, india, asia, marekani au ulaya.
Kuuza kiwanja cha kiwanda kwa 30,000 au 50,000 kwa square meter ni UJINGA sana

Pakiwa na viwanda vidogo vingi vitaongeza ajira, na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.

Bei ya kiwanja cha kiwanda kwa ajili ya vijana inatakiwa iwe 1000 kwa sqm au ikiwezana iwe hata shilingi miatano kwa square meter. Ili vijana wawe na maeneo yao ya kuwa na viwanda vidogo hata kwa laki tano. Vijana watashirikiana kuzalisha bidhaa na kuuza. Hivyo kuongeza ajira kwa vijana

Mfano halisi
Hicho ni kiwanja cha kujenga kiwanda kinauzwa na serikali Kibaha Mkoa wa Pwani angalia bei ya kiwanja cha kiwanda kinauzwa 600m. Je kuna kijana au mtanzania wa kawaida anayeweza kununua tu eneo kwa 600m?
Hii sio sawa, bei ni 30,000 kwa sqm 1
Kama serikali ina nia ya dhati ya kuzalisha ajira wapunguze bei ya viwanja vya kujengea kiwanda kuwa 1000 kwa sqm au 500 kwa sqm. Vijana wanunue kwa bei ndogo wawe bize kuzalisha bidhaa na kuchakata bidhaa za kilimo, uvuvi, ufugaji, Madini n.k

Screenshot_20250226-104551~2.png

Mfano wewe ngara23 ukiambiwa utoe 600m kununua kiwanja cha kiwanda unayo hiyo hela?
 
Vijana wengi wapo idle hawana kazi wana bet tu
Naomba serikali iondoe Kodi kwenye uingizaji wa mashine za uzalishaji

Vile vile Kuna ukiritimba wa uagizaji hasa wa zana za kilimo na pembejeo, Kuna matajiri wanapata vikwazo wakitaka kuagiza, maana Kuna viongozi wa serikali ndo wana hiyo nafasi ya kuagiza na kuuza bei kubwa Kwa wakulima

Mfano China tractor ni million 3 ila kufika huku litauzwa million 10
Tractors zikiwa cheap ni rahisi kuwashawishi vijana kulima, Sasa ni ngumu kumshawishi kijana kutumia jembe la mkono

Mashine zingine kama za kufyatua matofali, kuoaka mikate, kupasua mawe, mashine za kutotolesha vifaranga n.k zikipatina Kwa unafuu wa bei zitawafanya vijana wajiajiri kirahisi

Serikali imeondoa Kodi kwenye taasisi za dini, yaani Leo askofu anaweza kuingiza magari ya kifahari 200 Bure ila kuingiza tractors ni Kodi kubwa mno ambayo unasababisha upatikanaji kuwa mgumu

Serikali ufikirie vijana na kuhakikisha hasa zana na pembejeo za kilimo zinapatikana kirahisi
WAZO Zuri kabisa China kuna machine za kuzalisha chochote unachowaza tena kwa bei nafuu tatizo linakuja kwenye kodi zetu hapo bandarini.
 
Binafsi huwa naona Serikal haiko tayar kumsaidia mwananchi wa Kawaida, Maana kwa Nchi Zetu za Kiafrika tunajua fika kuwa kama watu wake watakuwa na Uchumi Mkubwa basi ni wazi kuwa hawatawatalawa. Maana kwa Nchi Kama Tanzania Mpaka karne hii kutegemea Mvua kwenye Kilimo ni aibu kubwa. Nchi imejaaliwa maziwa na Mito ambayo haikauki Mwaka mzima lakin bado hatuna Scheme za Kutosha za Umwagiliaji.
 
Back
Top Bottom