Serikali iondoe vibanda vilivyo Mbele ya Biashara nyingine Kariakoo, hali mbaya

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
9,753
Reaction score
10,747
Hawa machinga wanatutafutia ugomvi sisi wafanyabiashara wa maduka.

Kumbuka Wenye Fremu wanalipa Kodi TRA tutashindwa kulipa Kodi kwa style hii.

Serikali waliangalie hili Jambo kwa upana zaidi.

Hapa mteja anapita wapi kuja dukani wakati duka halionekani Kodi za pango ni zaidi ya milioni kwa mwezi tunapata shida Sana kufanya biashara.


 
Kiukweli Machinga wanakera sanaa, na wakiguswa kidogo tuu wanakimbilia kujiona wanyonge wa mitaji midogo huku wanaumiza wenzao.

Mwenzako analipa kodi 3M unakuja kumuwekea kichanja chako kwenye mlango wa biashara yake, na pengine bidhaa ile ile anayouza kwenye fremu wewe unauza kwa bei ya debe.

Nchi haiwezi kuendeshwa kwa huruma, Serikali iondoe hawa watu, ni kero si tuu kwa wauzaji bali hata kwa wateja wengine na wapita njia.
 
Wapite kwenye vibaraza, au duka lako halina kibalaza?!
 
Wanyonge wa kipindi cha Mwendazake, na wakiguswa watatoa sababu mwendazake kafa ndio wananyanyaswa.
 
Watu wanalipa frame halafu mwingine anakuja kukuziba kwa mbele, sio sawa.

Lakini pia, kama tunataka kuwa na style ya maisha ya kustaarabika, basi tuamue kwa dhati, kama Machinga complex sasa hivi wanaishi popo tu mule, hii maana yake nini?!
 
Kutengenezwe utaratibu mzuri kwa wamachinga kufanya biashara zao,hivi ubunifu kuhusu hawa watu kufanya biashara zao kwa ubora zaidi umeshindikana kabisa au ni uvivu tu wa kufikiri...?
 
Wanatakiwa watengewe sehemu mahalum kwa ajili ya kufanya biashara zao na ili likifanyika sisi wananchi tuhamasishane kama tunanunua bidhaa kwa Machinga basi twende hayo maeneo waliyotengewa, wale watakao endelea kukaa maeneo yasiyo rasmi tusinunue bidhaa zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kiukweli hii sio sawa....kodi anayolipa mtu wa ndani ya duka na huyo Machinga ni tofauti kabisa... kwa kweli ni uonevu mkubwa.
 
Ila kiukweli hii sio sawa....kodi anayolipa mtu wa ndani ya duka na huyo Machinga ni tofauti kabisa... kwa kweli ni uonevu mkubwa.
Ni wakati sasa kuwaondoa
 
Chadema walitangaza ikifika tarehe 18/05 watawatoa machinga wote lakini wameshindwa na kulegea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…