Serikali iondoe vibanda vilivyo Mbele ya Biashara nyingine Kariakoo, hali mbaya

Serikali iondoe vibanda vilivyo Mbele ya Biashara nyingine Kariakoo, hali mbaya

Hao watu ni wengi, na tayari maisha yao yapo hapo.
Inatakiwa kabla ya kuwaondoa watafutiwe eneo ambalo watapata wateja kama ilivyo maeneo waliyopo sasa. Kusema huruma haihitajiki kisa ni maendeleo ya nchi tutakuwa tunajaribu kufufua ukatili ambao tunajitahidi kuuzika.
Hao wana familia, kuwaondoa hapo ni sawa na kuanza kuwalaza njaa.
Hebu jaribu wewe ulale njaa kabla haujapendekeza mwenzako alale njaa. Tuache ukatili.
Walakini hayo maduka hayajazibwa na hivyo vibanda kiviile,, mtu akitaka kuingia dukani mbona anaingia tu??
Kulisha family kisiwe kisingizio cha kuvunja sheria, watu wamewekeza pesa zao kwenye maduka wao wana panga mbele huo ustarabu wa wapi
 
Halafu watu wanaowatete hawa kunguni hawana biashara wanayofanya, hata kama wanafanya hawafungua biashara mahali ambayo machinga wanapenda kukaaa, Ukiwapo huku katikati ya machinga halafu uone jinsi walivyo na ujinga mwingi kichwani unaweza ua, Wengine wanakaa hapo kwenye njia ya kuingia Dukani, halafu wanajifanya hawajui kama kuna duka kwa nyuma yao, yan huu ni ujinga wa kiwango cha lami,Maguful baada ya kuona wafanyabiashara hawana muda nae akaona awaruhusu machinga kwa kigezo cha unyonge kuziba njia za miji na masoko ya bidhaa, Utawala wa samia naona nao wanajingata ngata hakuna mwenye sauti ya kukemea huu ujinga kisa Mwendazake.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Dawa ya hili tatizo ni ndogo sana sana!! Wafanyabiashara wa maduka wangegoma kulipa kodi miezi mitatu tuuu serikali ingenyooka mbona!?? FFU wangeingia kazini fasta !!!
 
Kwakuwa ulaya wanafanya upuzi huu na sisi tufanye sio
mkuuu hata ulaya kuna machinga na watu wanafanya biashara pembeni mwa barabara ustarabu unaoutaka ni upi
 
Kariakoo machinga wamejazana kila sehem kila uchochoro, mpaka kero uchafu umetapakaaa kwa ajili yao.
Pia wengine kati yao diyo wezi wadokozi wamejibanza kwenye kivuli cha wengi.

Pia barabara zote wametandika vitu vyao chini, mbele ya maduka ya watu wengine, wanauza hawatoi risiti, ukiuziwa kitu feki hauna uhakika kama kesho muuzaji utamkuta pale alipokuuzia sababu Machinga wanauza vitu mikononi ni kero tupu bora duka una uhakika ukienda ukirudi unalikuta,

Kujaa kwa hao jamaa njia zote kunaleta kero sana na inapelekea uvunjaji wa haki ya msingi ya matumizi ya barabara kwa watu wote.

Hizi huruma kwa wamachinga kisa ndo wapiga kura ni upuuzi sana na wao hawachangii chochote zaidi ya kero kwa wengine na kuchafua mazingira na kuharibu miundo mbinu, imefika hatua kariakoo kila sehem ni harufu za ovyo ovyo, aisee naunga mkono hoja kwa hasira sana nikiwa mmoja ya wakereketwa wa machinga.
 
Sio Kariakoo tu, nadhani jiji lote kwa sasa ni kama halina mwenyewe..ukienda kule CBD pamekua kama mbagala.. yani sehemu za kutembea hakuna siku hizi,, wamejaa wao tu.. Tunajua ni kutafuta riziki ila inabidi waandaliwe utaratibu maalum
 
Hao watu ni wengi, na tayari maisha yao yapo hapo.
Inatakiwa kabla ya kuwaondoa watafutiwe eneo ambalo watapata wateja kama ilivyo maeneo waliyopo sasa. Kusema huruma haihitajiki kisa ni maendeleo ya nchi tutakuwa tunajaribu kufufua ukatili ambao tunajitahidi kuuzika.
Hao wana familia, kuwaondoa hapo ni sawa na kuanza kuwalaza njaa.
Hebu jaribu wewe ulale njaa kabla haujapendekeza mwenzako alale njaa. Tuache ukatili.
Walakini hayo maduka hayajazibwa na hivyo vibanda kiviile,, mtu akitaka kuingia dukani mbona anaingia tu??

Wanao wazibia maduka yao wanayolipa kodi ua pango na yanayotozwa kodi na TRA sio binadam wenzao? Wao hawanafamilia?
 
hao ukiwagusa ni msala. . Mkurugenzi wa Jiji alijaribu kutikisa kidogo akawapa siku kadhaa waondoe vibanda vyao aisee akaitwa Ikulu fasta na kupigwa stop ndomana ile inshu ikaishia hewani
 
hao ukiwagusa ni msala. . Mkurugenzi wa Jiji alijaribu kutikisa kidogo akawapa siku kadhaa waondoe vibanda vyao aisee akaitwa Ikulu fasta na kupigwa stop ndomana ile inshu ikaishia hewani
Huo mi upuuzi sana hatuwezi kuwa nchi wa waachuuzi kila kona mji lazima kuwe na utaratibu
 
Dawa ya hili tatizo ni ndogo sana sana!! Wafanyabiashara wa maduka wangegoma kulipa kodi miezi mitatu tuuu serikali ingenyooka mbona!?? FFU wangeingia kazini fasta !!!
Wenye maduka wote wafunge maduka wawe machinga
 
Hawa machinga wanatutafutia ugomvi sisi wafanyabiashara wa maduka.

Kumbuka Wenye Fremu wanalipa Kodi TRA tutashindwa kulipa Kodi kwa style hii.

Serikali waliangalie hili Jambo kwa upana zaidi.

Hapa mteja anapita wapi kuja dukani wakati duka halionekani Kodi za pango ni zaidi ya milioni kwa mwezi tunapata shida Sana kufanya biashara.

View attachment 1798116
Hatari
 
Msichojua ni kwamba, hukai mbele ya duka la mtu bure,lazima ulipe.

Na ni marufukua kuuza bidhaa anayouza mwenye duka, labda iwe ni boss mmoja.
 
Back
Top Bottom