SoC04 Serikali iongeze bajeti ya vifaa tiba na dawa kwa magonjwa ya figo na saratani kuwawezesha wagonjwa kupata huduma ya matibabu bure kwa asilimia 100

SoC04 Serikali iongeze bajeti ya vifaa tiba na dawa kwa magonjwa ya figo na saratani kuwawezesha wagonjwa kupata huduma ya matibabu bure kwa asilimia 100

Tanzania Tuitakayo competition threads

Alubati

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2016
Posts
6,535
Reaction score
14,840
Gharama kubwa ya tiba ya magonjwa ya saratani na figo nchini zinasababisha baadhi ya wagonjwa kuacha tiba sahihi hospitalini na na kutumia dawa za kienyeji ambazo zinachangia vifo.

Pamoja na jitihada za serikali kuboresha huduma eneo la magojwa hayo kwa kutoa msamaha wa matibabu kwa baadhi ya wagonjwa lakini bado gharama za matibabu zipo juu sana kiasi kwamba si rahisi kwa wagonjwa wenye kipato cha chini kuweza kuzimudu, kwakuwa msaada huo ni mdogo kulinganisha na idadi kubwa ya wagonjwa wenye uhitaji.

Wananchi wengi wana kipato kidogo kulinganisha na gharama kubwa za magonjwa haya,na si wote wanahudumiwa na mfuko wa Taifa wa bima ya afya. Mfano.. gharama za kusafisha figo nchini ni kati ya shilingi za Tanzania kati ya 250000 hadi 300000 kwa siku hivyo kama mgonjwa atasafishwa mara tatu kwa wiki ni shilingi kati ya 750000 hadi 900000, ni kubwa sana kwa watanzania wengi.

Hali hii pia ipo kwenye magonjwa ya saratani ambayo matibabu yake ni gharama kubwa mno kulingana na aina ya saratani na njia ya matibabu itakayotumika kwa mgonjwa,familia nyingi na kaya za watanzania ni masikini kuweza kumudu gharama hizi kubwa.katika kujaribu kupambania wagonjwa wao hulazimika kutumia kila walichonano katika matibabu ya wagonjwa wao kitu kinachowazamisha kwenye dimbwi la ufukara mara dufu.

Hivyo napendekeza Tanzania kati ya miaka 5 hadi 25 ijayo serikali kupitia wizara ya afya na kushirikiana na wadau, asasi za kiraia, wafadhili mbalimbali kuongeza bajeti ya vifaa tiba na dawa kwa magonjwa ya saratani na figo ili kuweza kuwaondolea wananchi wote gharama za matibabu kwa asilimia 100.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom