Upo sahihi lakini kama bado hatuna katiba ndio useme wasilinde nchi?
Ulinzi wa nchi ni dhana pana sana na nadhani tunapaswa kufanya tafiti za kina kupata ufahamu wa kudadavua Kwa usahihi .
Ulinzi wa nchi kiuchumi..Kwa nini watanzania wengi bado maskini miaka 60 baada ya uhuru licha ya utajiri wa rasilimali?.Kwa kandarasi kubwa Za ujenzi wa miundombinu zinatolewa Kwa makampuni ya nje hasa State owned enterprises Za China?
Kijamii:Je Tupo salama dhidi ya intrusions mbalimbali za maadui wa kijamii? Ushoga,Virutubisho kwenye vyakula,Vinywaji,Vyandarua vya misaada ,Madawa ya kilimo,Mifugo..Chanjo..Pombe..Betting’s..Tunatalaji kuwa na kizazi cha namna gani after 50 years
Kisiasa:Je mfumo uliopo unasaidiaje kufanikisha upatikanaji wa wanasiasa wenye Upeo mkubwa zaidi wa kusaidia taifa kusonga mbele Kiuchumi,Kijamii,Kisayansi?..Rushwa-Takrima..Ununuzi wa vyeo..
Naamini idara inafanya kazi kubwa licha ya changamoto za kimazingira lakini haitoshi..Investment kubwa ifanyike kwenye faculties mbambali zenye risks Kwa nchi.
Katiba:Mamlaka thabiti Kimuundo/kimajukumu/na wajibu viwekwe ndani ya katiba Kwa kuzingatia matakwa ya nchi Kwa miaka 50 na 100 ijayo..Haswa ktk kupata maendeleo ya kweli..Kuyalinda maendeleo husika sambamba na rasilimali Kwa faida ya vizazi vilivyopo na vijavyo.
Nadhani litaimarisha ushupavu wa watendakazi,nidhamu,umakini,ubobevu,weredi..Na ikibidi iitwe Taasisi ya Usalama wa Taifa..Wawe watendaji zaidi kupitia miiko,misingi,taratibu,Kanuni zao,Desturi zao..Wasiingiliwe,Wasivurugwe,Wasisukumwe kisiasa,Wasichangamane kisiasa..