MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Nichukue nafasi hii kumpongeza ndugu LIKUD kwa jitihada zake za kuziheshimisha shule za serikali ingawa sio kwa njia nzuri sana inayokubalika. Kuziinua St Kayumba kwa kuziponda EMs sio namna sahihi kwa sababu hata EMs ni za watanzania kwa ajili ya watanzania. Kwa pamoja EMs na Kayumba ziko kwa ajili ya Tanzania bora. Ila kwa akili kubwa nimeshaona Mzee Likud ana nia njema tu. Binafsi nimesoma shule za serikali mwanzo hadi mwisho. Std one hadi University.
Mimi nimesoma wakati ambapo hakukuwa na shule za kata. Matabaka haya yaliyopo kwa sasa hayakuwepo. Kwa wakati tuliopo kuna matabaka ndani ya shule za serikali. Kuna shule zinaitwa za kitaifa na shule zinazoitwa za kata. Hizi ni dunia mbili tofauti ndani ya serikali moja. Kwenye shule za kitaifa kuna miundombinu ya kueleweka wakiwemo waalimu wa kutosha huku kwenye shule za kata kukiwa na mapungufu mengi ikiwemo uhaba wa waalimu.
Kibaha, Moshi Tech, Ifunda, Ilboru, Mzumbe, Bwiru, Kantalamba, Tanga, Weruweru, Ashira, Korogwe girls, Karatu Old Moshi na zingine kongwe zinazoitwa za kitaifa ziko tofauti kabisa na shule za kata kama Oljoro, Mzimuni, Oljoro namba 5 na zingine. Haihitaji utafiti wowote kujua kuwa mwanafunzi wa Ashira girls ana nafasi kubwa ya kufanya vizuri kulinganisha na Oljoro sec. Hizi ni dunia mbili tofauti.
Mwanafunzi wa Ashira akiamka bwenini asbh anafanya kupiga hatua chache kwenda darasani. Huyu wa Oljoro akiamka asbh lazima awahi stendi ya Mirongo pale Mbauda kupanda lori la mchanga linaloenda kubeba mchanga Mirongoine. Kutoka Mbauda hadi Oljoro sec ni mwendo wa kama dakika 20 kwa lori.. mvua ikinyesha lazima imnyeshee huyu mtoto. Yaani ni huzuni.
Kuna mengi ya kuandika ila najua serikali ya Mama Samia itafanyia kazi kupunguza hili tabaka linalokua kwa kasi.