Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Juzi nimesikia NIHF ipo karibu kufirisika. Waziri anasema gharama za kutibu magonjwa yasiyoambukizwa ni kubwa sana. Ni magonjwa gani hayo yasiyoambukizwa?
Makubwa ni Kisukari, figo na high blood pressure. Haya kwa sehemu kubwa husababishwa na ulaji mbovu na sedentary lifestyle na yanahusiana sana. Matatizo mengi ya figo huletwa na kisukari.
Sasa kwa sehemu kubwa ulaji wa sukari na mafuta ndiyo visababishi vikubwa vya shida hiz. Inasemwa kuwa binadamu hakuumbwa kula sukari na mafuta kama anayokula leo.
Mambo hayo yana madhara kuliko vitu vikivyozoeleka kuwa na madhara kama pombe, sigara au bangi. Na mbaya zaidi, watu weusi tuna hatari zaidi ya kupata visukari na BP, lakini tumeiga ulaji wa kizungu wa mafuta na sukari nyingi.
Ni vyema, ili kuokoa jamii, serikali ikapiga marufuku soda na vinywaji vingine vilivyoongezwa sukari. Ikishindikana hilo, basi ilazimishe watengenezaji wa bidhaa hizo waweke onyo kama ilivyo kwenye sigara na pombe.