Serikali ipige marufuku soda na vinywaji vyote vilivyoongezwa sukari

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Juzi nimesikia NIHF ipo karibu kufirisika. Waziri anasema gharama za kutibu magonjwa yasiyoambukizwa ni kubwa sana. Ni magonjwa gani hayo yasiyoambukizwa?

Makubwa ni Kisukari, figo na high blood pressure. Haya kwa sehemu kubwa husababishwa na ulaji mbovu na sedentary lifestyle na yanahusiana sana. Matatizo mengi ya figo huletwa na kisukari.

Sasa kwa sehemu kubwa ulaji wa sukari na mafuta ndiyo visababishi vikubwa vya shida hiz. Inasemwa kuwa binadamu hakuumbwa kula sukari na mafuta kama anayokula leo.

Mambo hayo yana madhara kuliko vitu vikivyozoeleka kuwa na madhara kama pombe, sigara au bangi. Na mbaya zaidi, watu weusi tuna hatari zaidi ya kupata visukari na BP, lakini tumeiga ulaji wa kizungu wa mafuta na sukari nyingi.

Ni vyema, ili kuokoa jamii, serikali ikapiga marufuku soda na vinywaji vingine vilivyoongezwa sukari. Ikishindikana hilo, basi ilazimishe watengenezaji wa bidhaa hizo waweke onyo kama ilivyo kwenye sigara na pombe.
 
+
 
Upo sahihi ila Asilimia kubwa ya vyakula vinavyotuzunguka ni vichochezi vya Sukari mwilini zaidi ya sukari yenyewe...

Sioni mazingira rahisi Mbongo wa kawaida anachomoa siku bila kula Carbohydrates - Starch - Glucose-Sugar.

Kikubwa ni At least ku balance, sio tuu vinywaji bali na chakula piaa.
 

Kweli kabisa magonjwa sugu matibabu Yake yana gharama kubwa sana na magonjwa sugu yanaua sana ,ila kwa sasa kuna tiba ya kutibu magonjwa hayo Kama moyo,kisukari,presha,kansa aina zote,figo,ini ,tezi dume ,bawasiri,na maradhi mengine zaidi ya 165 ambaye anaitaj hiyo tiba aje kwa inbox nimuelekeze hiyo tiba inapopatikana
 

Chief uko sayari ya mars au? Hakuna direct connection ya hizo sukari na matatizo hayo, magonjwa yanayotokana na life style au yasiyoambukiza (NTDs$ yana multiple causes.

Ni jukumu la serikali kutoa elimu ya ufahamu ili ukitumia utumie kwa akili lakini at your own risk.

Ni vizuri kutokuwa conclusive kwenye mambo ya kitaalamu ambayo huna ufahamu nayo.
 
Bonge la ushauri
 
Ni kweli magonjwa yasiyoambukizwa yanasababu nyingi. Lakini sababu kubwa kwa sasa ni ulaji mbaya na sedentary lifestyle. Hizo sukari sukari zinasababisha moja kwa moja. Sukari zinaleta unene unaleta matatizo ya moyo, unene unaleta insulin resistance na kisukari aina ya pili. Kisukari kinaleta shida ya Ini nk nk.

Ulaji wa sukari na mafuta mengi, ukichangia na maisha ya kukaa tu ni visababishi vikubwa vya magonjwa yasiyoambukiza. Kwani we shuleni kwako ulifundishwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…