Mwamba Kizota
New Member
- Apr 12, 2021
- 2
- 1
Story of Change kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan. Naanza kwa nukuu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Aliwahi kusema ili tuendelee tunahitaji mambo manne. Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora. Katika haya nachagua Ardhi na Watu kukusanya fedha ya kutosha ikiwa ni mbadala wa Tozo zinazoonekana kuwa kubwa. Najua kwa dhati kabisa na natambua umuhimu wa kujenga uwezo wa kifedha ili tujiletee maendeleo. Mjadala uliopo ni wapi tunapata pesa katika mazingira rafiki kama ilivyo dhamira yako.
Wakati fulani hata Spika wa Bunge ameomba mawazo mbadala kama inawezekana. Tozo ni wazo zuri na ambalo tumeliiga kwa wenzetu, lakini wenzetu hao hawana ardhi ya kutosha kama ilivyo TANZANIA. Kwa maana hiyo utuuzie ARDHI sisi wananchi wako. Maadui wakubwa tangu enzi za Mwalimu ni Ujinga, Maradhi na Umaskini-ambao umewafanya wachache kumiliki Ardhi. Mheshimiwa Rais, rahisisha zoezi la kumiliki ardhi KWA MALIPO KIDOGO KIDOGO. Tukiamua tunaweza.
Chukulia kwa mfano; Ukiwa na viwanja vya makazi na biashara vipatavyo Milioni Tano (5,000,000) tu kwa nchi nzima vyenye wastani wa Tsh. 700,000 kila kiwanja. Ukiviweka sokoni kwa malipo ya mkupuo ni WACHACHE wenye UWEZO watakaweza kuvinunua, lakini ukivitangaza na ukahamasisha vya kutosha kwa malipo KIDOGO KIDOGO mfano Tsh. 50,000 kila mwezi. Utakusanya Tsh. Bilioni 250 kila mwezi kwa muda wa miezi 14 hivi. Hiki kiwango cha fedha ni kingi sana na huu ni mfano tu.
Watanzania wengi wana kiu ya kumiliki ARDHI lakini uwezo wa kulipa kwa mkupuo ni mdogo. Elfu hamsini iwe juu au chini yake ni hamasa kubwa na naamini utapata mwitikio wa kutosha. Wizara ya Ardhi kwa kushirikiana na Halmashauri zetu watumie wazo hili vizuri, binafsi naamini litasaidia. Ukikusanya fedha kwa njia hii na ukaridhika basi upunguze tozo (sio kuziondoa kabisa) ili tuboreshe huduma za jamii.
Wananchi tunadhaminika. Kumbuka kwenye uchaguzi mkuu tulidhaminika kwa Kitambulisho cha Mpiga Kura, Kitambulisho cha Uraia, Hati ya Kusafiria, Leseni ya Udereva. Hata Jaji Mkuu alipata kusema mahali kwamba kitambulisho cha Taifa kisaidie kuwapa watu dhamana hata kwa mashtaka madogo. Tumilikishe ARDHI kwa malipo kidogo kidogo kwa dhamana hizo, hii itaamusha ARI ya kufanya kazi na itakuwa ni safari ya kuchochea viwanda vya Saruji, Mabati, Nondo...kuzalisha kwa wingi ili watu wajenge. Itakuwa safari kwa Serikali kuweka miundo mbinu ya Maji, Umeme na Barabara. Kwa ujumla utaweka HESHIMA kwa wananchi wenye kiu ya kumiliki ARDHI lakini hawana uwezo wa kulipa kwa mkupuo mmoja.
Tazama, Bilioni250 ni karibu madarasa 17,000 yenye thamani ya Tsh.15,000,000 kila moja zikiwemo nguvu za wananchi. Bilioni 250 ni sawa na Zahanati 625- Zahanati karibu 4 kwa kila Halmashauri kwa kila mwezi zenye thamani ya Tsh Milioni 400. Wazo hili naliona jema. Tuwekee utaratibu mzuri ili tujiletee maendeleo kwa kutumia ARDI yetu. Naomba kuwasilisha.