kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Waziri mkuu tengeneza mfumo unaofanyakazi wenyewe hukohuko makazini bila wewe kulazimika kuzunguuka n kutatua kero za wananchi kwenye ziara zao. Watanzania wooote wanazo kero zao lakini ama hawana muda wa kuja ofisini kwao, ni wengi kuliko muda ulionao wa kueleza kero zao au hujafika kwao waseme kero zao kama ulivyofika huko ulikotembelea.
Asilimia 99% ya kero za wananchi zinasababishwa na watoa huduma, yaani watu walioajiriwa na kuteuliwa kuwahudumia wananchi. Kuna kero wanakwambia wewe ambazo zilipaswa kutatuliwa na mtendaji kata tu, tarafa au mkurugenzi wa wilaya tu. Lakini watoabhuduma hawa wamekata tamaa kabisa kabisa kabisa kabisa kuweza kutoa huduma safi kwa wananchi.
Viongozi na watumishi wenu hawana morali ya kazi; mishahara midogo sana na makato ya kodi (PAYE) yenye kikokotoo juu yake. Hawapewi nyumba, chakula kazini wala usafiri wa kwenda na kurudi kazini. Matibabu yao na shule za watoto wao ni kama watu wengine tu.
Thamani ya shilingi imeshuka, mfumko wa bei umepanda na maisha yamepanda lakini mtumishi mshahara wake ni kidogo sana na makato makubwa na hata akistaafu kikokotoo kiko palepale. Hakuna mtu mjinga atatabasabu kwa mteja huku tumboni hakuna kitu.
Watumishi na viongozi lazima watabuni njia za kupata chakula, usafiri, nyumba, na ada ya watoto wao mtake msitake kabla hawajastaafu kazi. Na njia zenyewe ni ama kutumia muda wa kazi kufanya kazi zao, kuiba mali ya mwajiri au kuhamisha kasima ya mradi kulipana posho au rushwa kazini.
Ziara zako hizo ni nzuri lakini utafute suluhisho kwa wananchi wote kwasababu kero ziko kila sekta na kila kitongoji nchini na huwezi kuzitatua wewe kununa, kufoka wala kufukuza watumishi. Lazima ushuhulikie the underlying and basic causes of the problems badala ya kuhangaika na the immediate causes of the problem.