Serikali irejeshe kwanza pesa ilizowapora wafanyabiashara....

Serikali irejeshe kwanza pesa ilizowapora wafanyabiashara....

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Serikali ya awamu ya sita chini ya mama Samia Suluhu imeanza kazi kwa kutoa wito kwa wafanyabiashara wote hapa Tanzania na nje ya Tanzania kurudi na kuendelea na biashara hapa nchini baada ya baadhi yao kufilisika, kususa, kukimbia au kupunguza mitaji tangu utawala wa Magufuli aingie madarakani.

Wito huo wa serikali ya mama Samia umepokelewa kwa mitazamo tofauti ambapo wengi wa wafanyabiashara wakisema tamko hilo huenda ni danganya toto kwa kuwa wanaotoa wito huo ni watu wale wale waliokuwa ni sehemu ya utawala wa Magufuli uliowakatili vibaya kibiashara, hivyo ni mapema sana kuamini na wao kuchukua hatua za kurejea kwa nguvu kufanya biashara.

Na sasa ushauri umetolewa kuwa, kwa kuwa serikali hii inakiri wazi kuwa, haki haikutendeka na wala sheria hazikufuatwa ipasavyo wakati wa kuwafilisi wafanyabiashara, ni muda muafaka sasa kwa serikali kuanza mara moja mchakato wa kuanza kwanza kuwarejeshea wafanyabiashara pesa zao walizoporwa pasipo uhalali ili kurejesha imani na maafikiano baina yao na serikali.

Wito huo umelenga kumfikia Rais Samia Suluhu, makamu wa Rais (Philip Mpango) na waziri wa fedha (Mwigulu Nchemba)
 
mama alisema mkakusanye mapato bila kutumia nguvu wala kuwachukulia pesa zao kwenye account japo inaruhusiwa kisheria
 
Serikali ilipe Pesa za mifuko ya jamii NSSF na PSSSF

Watu walipwe mafao yao.

CCM wanapora fedha kufanyia Kampeni
 
Back
Top Bottom