Serikali irejeshe saikolojia ya wanafunzi wa shule ya msingi Mbezi Juu ili wendelee vyema na masomo yao

Pendragon24

Member
Joined
Aug 8, 2018
Posts
68
Reaction score
97
Siku ya alhamisi tarehe 19.09.2024 katika shule ya msingi ya Mbezi juu palitokea tukio la mwanafunzi mmoja wa kiume wa darasa la tatu kutumbukia ndani ya shimo la choo wakati alipokwenda kujisaidia majira ya mchana.

Shule ya msingi Mbezi juu ipo katika kata ya Ndumbi mtaa wa Mbezi mtoni ndani ya jimbo la Kawe wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Jitihada za kuokoa uhai wa mtoto huyo zilifanyika kwa ushirikiano mkubwa wa baadhi ya wananchi na wanafunzi wa shule ya sekondari ya mbezi juu iliyopo karibu na choo cha shule ya msingi na kufanikiwa kumtoa mwanafunzi huyo aliyekuwa ndani ya tundu hilo la choo.

Mtoto alipata majeraha mbalimbali katika sehemu zake za mwili na kuvunjika baadhi ya vidole vya mikononi alipokuwa akijinusuru ili kuokoa uhai wake.

Baada ya kufanikiwa kwa zoezi la uokoji, majira ya saa mbili za usiku askari wa jeshi la zimamoto walifika katika eneo la tukio na kukagua kama kuna mwanafunzi mwingine yeyote ndani ya shimo hilo la choo cha shule aweze kupewa msaada, wakiwa na gari la zimamoto na kijiko (katapila) kilichotumika kufukua na kuezua mabati ya choo hicho.

Katika tukio hilo pamoja na uokoaji kufanyika lakini bado kuna shida kubwa ya kisaikolojia iliyosalia ndani ya wanafunzi,wazazi,walimu na jamii ambayo ilishuhudia kile kilichotokea kwa mtoto huyo aliye nusurika kifo.

Kwa kawaida tukio kama hilo litabaki ndani ya vichwa vyao likizunguka na kuwajaza hofu na wasiwasi mkubwa siku zote wakiwa katika eneo la shule na hasa wakitazama choo kilicho bomolewa ili kuokoa maisha ya mwanafunzi mwenzao na kuzungushiwa utepe mwekundu (red tape)

Hivyo serikali isihishie tu kutoa msaada wa ujenzi wa choo kipya shuleni hapo lakini pia ihakikishe saikolojia ya wanafunzi iliyoharibiwa na tukio hilo inalejea ili waendelea kuwa na furaha na wazingatie masomo yao kikamilifu bila hofu katika robo muhula ya mwisho ya mwaka wa masomo yao.

Unaweza kuchukulia tukio hili ni la kawaida sana lakini fikiria saikolojia ya mwanafunzi aliye tumbukia ndani ya shimo hilo na wanafunzi wenzake zilivyo baada ya tukio hilo?

Fikia wewe ndio mwalimu wa shule hiyo wazazi wanakutazamaje juu ya usalama wa watoto wao wakiwa shuleni?

Je, mzazi atakuwa na wasiwasi na hofu kiasi gani anapo mruhusu mtoto wake aende shule ili hali hana uhakika na usalama wake huko anakokwenda?

Mwisho, tunaitaka serikali kusitisha haraka ujenzi wa vyoo vya shimo visivyo jengelewa na vilivyojengelewa kwa wanafunzi sio tu wa shule ya msingi lakini hata sekondari katika maeneo ya shule kote nchini.

Maana katika nyakati za mvua mvua ardhi inatabia ya kutitia na kuzama kisha kuleta maafa makubwa, hivyo vyoo vya shimo si salama kwa wanafunzi wa shule popote pale nchini.

~SAIDIENI HII JAMII
 
Siku ya alhamisi tarehe 19.09.2024 katika shule ya msingi ya Mbezi juu palitokea tukio la mwanafunzi mmoja wa kiume wa darasa la tatu kutumbukia ndani ya shimo la choo wakati alipokwenda kujisaidia majira ya mchana.

Shule ya msingi Mbezi juu ipo katika kata ya Ndumbi mtaa wa Mbezi mtoni ndani ya jimbo la Kawe wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.

Jitihada za kuokoa uhai wa mtoto huyo zilifanyika kwa ushirikiano mkubwa wa baadhi ya wananchi na wanafunzi wa shule ya sekondari ya mbezi juu iliyopo karibu na choo cha shule ya msingi na kufanikiwa kumtoa mwanafunzi huyo aliyekuwa ndani ya tundu hilo la choo.

Mtoto alipata majeraha mbalimbali katika sehemu zake za mwili na kuvunjika baadhi ya vidole vya mikononi alipokuwa akijinusuru ili kuokoa uhai wake.

Baada ya kufanikiwa kwa zoezi la uokoji, majira ya saa mbili za usiku askari wa jeshi la zimamoto walifika katika eneo la tukio na kukagua kama kuna mwanafunzi mwingine yeyote ndani ya shimo hilo la choo cha shule aweze kupewa msaada, wakiwa na gari la zimamoto na kijiko (katapila) kilichotumika kufukua na kuezua mabati ya choo hicho.

Katika tukio hilo pamoja na uokoaji kufanyika lakini bado kuna shida kubwa ya kisaikolojia iliyosalia ndani ya wanafunzi,wazazi,walimu na jamii ambayo ilishuhudia kile kilichotokea kwa mtoto huyo aliye nusurika kifo.

Kwa kawaida tukio kama hilo litabaki ndani ya vichwa vyao likizunguka na kuwajaza hofu na wasiwasi mkubwa siku zote wakiwa katika eneo la shule na hasa wakitazama choo kilicho bomolewa ili kuokoa maisha ya mwanafunzi mwenzao na kuzungushiwa utepe mwekundu (red tape)

Hivyo serikali isihishie tu kutoa msaada wa ujenzi wa choo kipya shuleni hapo lakini pia ihakikishe saikolojia ya wanafunzi iliyoharibiwa na tukio hilo inalejea ili waendelea kuwa na furaha na wazingatie masomo yao kikamilifu bila hofu katika robo muhula ya mwisho ya mwaka wa masomo yao.

Unaweza kuchukulia tukio hili ni la kawaida sana lakini fikiria saikolojia ya mwanafunzi aliye tumbukia ndani ya shimo hilo na wanafunzi wenzake zilivyo baada ya tukio hilo?

Fikia wewe ndio mwalimu wa shule hiyo wazazi wanakutazamaje juu ya usalama wa watoto wao wakiwa shuleni?

Je mzazi atakuwa na wasiwasi na hofu kiasi gani anapo mruhusu mtoto wake aende shule ili hali hana uhakika na usalama wake huko anakokwenda...!?

Mwisho, tunaitaka serikali kusitisha haraka ujenzi wa vyoo vya shimo visivyo jengelewa na vilivyojengelewa kwa wanafunzi sio tu wa shule ya msingi lakini hata sekondari katika maeneo ya shule kote nchini.

Maana katika nyakati za mvua mvua ardhi inatabia ya kutitia na kuzama kisha kuleta maafa makubwa, hivyo vyoo vya shimo si salama kwa wanafunzi wa shule popote pale nchini.

~SAIDIENI HII JAMII
Tupo bize kudhibiti kina Lissu. Mambo ya Saikolojia kafanya wewe na mumeo
 
Huyo mwanafunzi itakuwa alipata mshtuko(shock) mkubwa sana.

Nikivuta picha nabaki na huzuni.
 
Back
Top Bottom