SoC04 Serikali iruhusu uwekezaji wa Sekta Binafsi kwenye Sekta ya Nishati na Maji nchini ili kutanua wigo wa uzalishaji na ushindani wa kihuduma

Tanzania Tuitakayo competition threads

mackj

Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
84
Reaction score
98
Tanzania tuitakayo ni yenye umeme wa uhakika na maji visivyokatika ovyo na kupunguza uzalishaji mali na kuendelea kuchochea umasikini miongoni mwa wananchi.

Umeme na maji kimekuwa ni kilio cha kudumu katika Taifa la Tanzania tangu uhuru licha ya kubarikiwa kuwa na vyanzo vingi vya maji vinavyozalisha umeme na kutumika kusambaza huduma ya maji safi kitu ambacho kinazua mijadala isiyo isha kila mwaka hasa katika nyakati za kiangazi.

Kuna nchi ambazo asilimia 90 ya ardhi yake ni jangwa lakini hakuna shida ya maji wala mgao wa umeme au kukatika kwa umeme kunakosababishwa na sababu yoyote ile, nchi hizo ni kama botswana misri n.k.

Hapa kwetu Kikwazo kinachopelekea kutokuwepo kwa umeme wa uhakika na huduma bora za maji ni mashirika ya UMMA kukabidhiwa dhamana ya kutoa huduma hizo, bila kuwepo na ushindani kutoka kwa sekta binafsi ambapo mashirika haya yanajisahau na kuridhika,na kuamini hakuna cha kupoteza na huku mzigo mkubwa wakitwishwa wananchi, kwa kutopata huduma wanazo stahili ikiwa wanalipa kodi

mfano katika sekta ya upatikanaji wa maji safi mikoa ya pwani, dar es salaam na Tanga wananchi wanaishi kwa kupata maji kwa mgao na sote ni mashahidi hata umeme umekuwa ni kilio cha muda ambacho imeisha kuwa sehemu ya maisha ya watanzania serikali imefanya jitihada kubwa kuondoa changamoto hizi kwa kujenga miundo mbinu thabiti kwa kuwekeza fedha nyingi lakini kutokana na ongezeko la idadi ya watu na makazi bado inakuwa nichangamoto kufikia malengo tarajiwa.

kwakuwa tegemeo kubwa la vyanzo vya nishati ni vile vile vya maji. Na maji hayo hayo ndiyo yanategemewa kwa mahitaji mfano mto ruvu ndio unaotumika kwa maji ya kutumia kwa shughuli za kibinadamu na wanyama, na kihansi vile vile na hata bwawa la mtera hivyo hivyo.

Nini kifanyike katika kutatua changamoto hii na kilio hiki kuwa historia kwa nchi

kuruhusu sekta binafsi mashirika na makampuni ya nishati duniani kuja kuwekeza katika sekta hizi muhimu ili kuleta ufanisi na ushindani wa kihuduma ambapo mashirika yatakuwa ni mengi na yenye mipango ya uzalishaji wa nishati na usambazaji wa maji kwa kutumia teknolojia mbadala na siyo tegemea vyanzo vilevile ambavyo mashirika ya umma Yamekuwa yakitumia kwa miongo kadhaa
Katika mpango huu serikali itatunga sheria ambayo itaongoza na kusimamia uzalishaji huu kwa kuzingatia matakwa na mahitaji ya nchi bila kuathiri mazingira na rasili mali asili kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.

Sekta binafsi zitawajibika moja kwa moja kwa shirika mama la tanesco na mamlaka za maji kupitia wizara zinazohusika ambapo kazi yao wawekezaji itakuwa nikubuni mbinu na vyanzo vipya vya nishati na maji, kuwekeza rasilimali fedha kwa maana ya mitaji, teknolojia na wataalamu, na kisha Tanesco kusamabaza umeme kwa wanachi kwa kushirikiana na makampuni hayo kwa mfumo wa (PPP) ili kuendelea kuipa uhai Tansco.

Nchi za afrika magharibi ambazo ni guinea, Niger, na Bukinafaso ni wazalishaji wakubwa wa madini ya uranium yanayotumika kutengeneza nyukilia ambayo pia inatumika kuzalisha umeme na makampuni ya wamarekani na wafaransa ndio wazalishaji wakubwa wa nishati ya umeme na nchi hizo zinapata faida kupitia kodi na umeme ni wa uhakika na viwanda vinapewa umeme bure ili kukuza uzalishaji na kuwapa faida wananchi kwa kununua bidhaa zinazozalishwa nchini kwa bei nafuu kama vile mbolea n.k

Aidha tanzania inavyo vyanzo vingi vya nishati kama vile upepo ambao unapatikana singida, dodoma na maeneo mbalimbali, kuna makaa ya mawe ambapo tayari tunayo migodi ambayo ni liganga na mchuchuma kuna madini ya Uranium pia.

Tanzania tuna jua la kutosha ambapo umeme wa sola unaweza kutosheleza kabisa uzalishaji wa umeme ambao unaweza kutumika mashambani kwa kuzalisha viuatilifu, madawa ya mifugo, uzalishaji na usindikaji wa mbegu bora na kupunguza utegemezi wa kutoa mbegu na mbolea nje ya nchi
siyo kwamba tanzania viwanda haviwezekani kujengwa pamoja na sera zetu za uwekezaji kuwa rafiki lakini changamoto ya umeme wa ukakika nayo ni kikwazo.

Maendeleo ya nchi nyingi duniani yamechochewa na sekta binafsi, mashirika ya uma yamekuwa yakikoswa ufanisi kutokana na kuhujumiwa zaidi ambapo sera ya nchi yetu, "serikali haifanyi biashara kazi ya serikali nikutoa huduma"

Lakini katika mashirika haya ya kuzalisha umeme na maji wamesahau kuwa hiyo ni biashara ambapo kwa kuzingatia ushauri huu tanesco na mamlaka za maji watakuwa watoa huduma katika nyanja ya usambazaji Huku mzalishaji atakuwa ni sekta binafsi

Jambo hili kwa nchi yetu si geni mfano sekta ya mawasiliano mwaka 2003 kupitia serikali ya awamu ya tatu Rais benjamini wiliam mkapa kupitia ilani ya uchaguzi ya 2000 aliahidi “kuimarisha sekta ya mawasiliano ili kutuingiza katika karne ya 21 ambapo sekta binafsi iliruhusiwa kuwekeza katika sekta ya mawasiliano mpaka leo tunaona nchi inaubunifu mwingi wa huduma za mawasiliano na ushindani ni mkubwa wa kihuduma na imerahisisha upatikanaji wa mawasiliano mpaka vijijini

Faida za sekta binafsi kuruhusiwa kuwekeza kwenye sekta ya umeme na maji

1. Kupunguza changamoto ya upungufu wa umeme wa mara kwa mara na kuliweka Taifa kwenye giza

2. Kuwa na uhakika wa maji safi muda wote kwani vyanzo vya maji vinavyotumika kuzalisha umeme vitakuwa na uhakika wa usalama wa maji ya kutumia kwa binadamu na wanayama kwakuwa umeme utakuwa unatoka katika vyanzo vingine kwa asilimia kubwa ukilinganisha na sasa

3. Bei ya nishati itapungua kwa kiasi kikubwa kwakuwa ushindani wa kutoa huduma utapelekea uzalishaji kuwa mkubwa.

4. Uzalishaji mali utaongezeka na pato la mtu mmoja mmoja litaongezeka na kupunguza umasikini

5. Utapunguza mfumuko wa bei kwa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi kwakuwa hakutakuwa na kisingizio cha gaharama za uzalishaji kuwa juu kutokana na kutumia majenereta

6. Kutakuwa na ongezeko la viwanda vidogovidogo vya kati na vikubwa vitakavyo zalisha ajira nyingi.

Ni matumaini yangu kwamba serikali itaweza kutumia ushauri na mawazo haya mtambuka na kutoka kwenye mawazo finyu ya kutegemea shirika moja tu la umeme lizalishe, lisambaze, na liuze.

Kwenye maji hivyo hivyo kitu ambacho kilikuwa nicha kizamani.

Asanteni.
Naomba kuwasilisha.
 
Upvote 4
Chapisho Zuri 👏
Asante mkuu tanzania ni yetu na umeme na maji ndio injini ya uchumi serikali haiwezi kufanya kila kitu yenyewe note "you always be safe if you have some one to blame"

huwezi kufikiri wewe, ubuni wewe, uchakate wewe, uzalishe wewe, uuze wewe, usambaze wewe, ukusanye madeni wewe, hapana.

serikali kwenye maeneo yenye kugusa maisha ya wananchi moja kwa moja km haya na yanayogusa uchumi endelevu wa nchi na watu wake, sekta binafsi ni muhimu sana unless other wise kuna kilichojificha kisichotakiwa kujulikana!

lakini km bandari na other strategic infrastructure tanzania zimepewa sekta binafsi kuendesha, hata hii sekta inabidi serikali ifikilie na kuchukua hatua za haraka.

ni haibu kwa taifa zama hizi technolojia na mageuzi ya kiuchumi chi bado tunachechemea kuwa proper power, na proper water supply huku tuna vyanzo vingi vya maji na umeme.😎
 
Tanzania tuitakayo ni yenye umeme wa uhakika na maji visivyokatika ovyo na kupunguza uzalishaji mali na kuendelea kuchochea umasikini miongoni mwa wananchi.

Umeme na maji kimekuwa ni kilio cha kudumu katika Taifa la Tanzania tangu uhuru licha ya kubarikiwa kuwa na vyanzo vingi vya maji vinavyozalisha umeme na kutumika kusambaza huduma ya maji safi kitu ambacho kinazua mijadala isiyo isha kila mwaka hasa katika nyakati za kiangazi.

Kuna nchi ambazo asilimia 90 ya ardhi yake ni jangwa lakini hakuna shida ya maji wala mgao wa umeme au kukatika kwa umeme kunakosababishwa na sababu yoyote ile, nchi hizo ni kama botswana misri n.k.

Hapa kwetu Kikwazo kinachopelekea kutokuwepo kwa umeme wa uhakika na huduma bora za maji ni mashirika ya UMMA kukabidhiwa dhamana ya kutoa huduma hizo, bila kuwepo na ushindani kutoka kwa sekta binafsi ambapo mashirika haya yanajisahau na kuridhika,na kuamini hakuna cha kupoteza na huku mzigo mkubwa wakitwishwa wananchi, kwa kutopata huduma wanazo stahili ikiwa wanalipa kodi

mfano katika sekta ya upatikanaji wa maji safi mikoa ya pwani, dar es salaam na Tanga wananchi wanaishi kwa kupata maji kwa mgao na sote ni mashahidi hata umeme umekuwa ni kilio cha muda ambacho imeisha kuwa sehemu ya maisha ya watanzania serikali imefanya jitihada kubwa kuondoa changamoto hizi kwa kujenga miundo mbinu thabiti kwa kuwekeza fedha nyingi lakini kutokana na ongezeko la idadi ya watu na makazi bado inakuwa nichangamoto kufikia malengo tarajiwa.

kwakuwa tegemeo kubwa la vyanzo vya nishati ni vile vile vya maji. Na maji hayo hayo ndiyo yanategemewa kwa mahitaji mfano mto ruvu ndio unaotumika kwa maji ya kutumia kwa shughuli za kibinadamu na wanyama, na kihansi vile vile na hata bwawa la mtera hivyo hivyo.

Nini kifanyike katika kutatua changamoto hii na kilio hiki kuwa historia kwa nchi

kuruhusu sekta binafsi mashirika na makampuni ya nishati duniani kuja kuwekeza katika sekta hizi muhimu ili kuleta ufanisi na ushindani wa kihuduma ambapo mashirika yatakuwa ni mengi na yenye mipango ya uzalishaji wa nishati na usambazaji wa maji kwa kutumia teknolojia mbadala na siyo tegemea vyanzo vilevile ambavyo mashirika ya umma Yamekuwa yakitumia kwa miongo kadhaa
Katika mpango huu serikali itatunga sheria ambayo itaongoza na kusimamia uzalishaji huu kwa kuzingatia matakwa na mahitaji ya nchi bila kuathiri mazingira na rasili mali asili kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.

sekta binafsi zitawajibika moja kwa moja kwa shirika mama la tanesco na mamlaka za maji kupitia wizara zinazohusika ambapo kazi yao wawekezaji itakuwa nikubuni mbinu na vyanzo vipya vya nishati na maji, kuwekeza rasilimali fedha kwa maana ya mitaji, teknolojia na wataalamu, na kisha Tanesco kusamabaza umeme kwa wanachi kwa kushirikiana na makampuni hayo kwa mfumo wa (PPP) ili kuendelea kuipa uhai Tansco.

Nchi za afrika magharibi ambazo ni guinea, Niger, na Bukinafaso ni wazalishaji wakubwa wa madini ya uranium yanayotumika kutengeneza nyukilia ambayo pia inatumika kuzalisha umeme na makampuni ya wamarekani na wafaransa ndio wazalishaji wakubwa wa nishati ya umeme na nchi hizo zinapata faida kupitia kodi na umeme ni wa uhakika na viwanda vinapewa umeme bure ili kukuza uzalishaji na kuwapa faida wananchi kwa kununua bidhaa zinazozalishwa nchini kwa bei nafuu kama vile mbolea n.k

Aidha tanzania inavyo vyanzo vingi vya nishati kama vile upepo ambao unapatikana singida, dodoma na maeneo mbalimbali, kuna makaa ya mawe ambapo tayari tunayo migodi ambayo ni liganga na mchuchuma kuna madini ya Uranium pia.

Tanzania tuna jua la kutosha ambapo umeme wa sola unaweza kutosheleza kabisa uzalishaji wa umeme ambao unaweza kutumika mashambani kwa kuzalisha viuatilifu, madawa ya mifugo, uzalishaji na usindikaji wa mbegu bora na kupunguza utegemezi wa kutoa mbegu na mbolea nje ya nchi
siyo kwamba tanzania viwanda haviwezekani kujengwa pamoja na sera zetu za uwekezaji kuwa rafiki lakini changamoto ya umeme wa ukakika nayo ni kikwazo.

Maendeleo ya nchi nyingi duniani yamechochewa na sekta binafsi, mashirika ya uma yamekuwa yakikoswa ufanisi kutokana na kuhujumiwa zaidi ambapo sera ya nchi yetu, "serikali haifanyi biashara kazi ya serikali nikutoa huduma"

lakini katika mashirika haya ya kuzalisha umeme na maji wamesahau kuwa hiyo ni biashara ambapo kwa kuzingatia ushauri huu tanesco na mamlaka za maji watakuwa watoa huduma katika nyanja ya usambazaji Huku mzalishaji atakuwa ni sekta binafsi

Jambo hili kwa nchi yetu si geni mfano sekta ya mawasiliano mwaka 2003 kupitia serikali ya awamu ya tatu Rais benjamini wiliam mkapa kupitia ilani ya uchaguzi ya 2000 aliahidi “kuimarisha sekta ya mawasiliano ili kutuingiza katika karne ya 21 ambapo sekta binafsi iliruhusiwa kuwekeza katika sekta ya mawasiliano mpaka leo tunaona nchi inaubunifu mwingi wa huduma za mawasiliano na ushindani ni mkubwa wa kihuduma na imerahisisha upatikanaji wa mawasiliano mpaka vijijini

Faida za sekta binafsi kuruhusiwa kuwekeza kwenye sekta ya umeme na maji

1. kupunguza changamoto ya upungufu wa umeme wa mara kwa mara na kuliweka Taifa kwenye giza

2.kuwa na uhakika wa maji safi muda wote kwani vyanzo vya maji vinavyotumika kuzalisha umeme vitakuwa na uhakika wa usalama wa maji ya kutumia kwa binadamu na wanayama kwakuwa umeme utakuwa unatoka katika vyanzo vingine kwa asilimia kubwa ukilinganisha na sasa

3.bei ya nishati itapungua kwa kiasi kikubwa kwakuwa ushindani wa kutoa huduma utapelekea uzalishaji kuwa mkubwa.

4.uzalishaji mali utaongezeka na pato la mtu mmoja mmoja litaongezeka na kupunguza umasikini

5. Utapunguza mfumuko wa bei kwa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi kwakuwa hakutakuwa na kisingizio cha gaharama za uzalishaji kuwa juu kutokana na kutumia majenereta

6.kutakuwa na ongezeko la viwanda vidogovidogo vya kati na vikubwa vitakavyo zalisha ajira nyingi.

Ni matumaini yangu kwamba serikali itaweza kutumia ushauri na mawazo haya mtambuka na kutoka kwenye mawazo finyu ya kutegemea shirika moja tu la umeme lizalishe, lisambaze, na liuze.

kwenye maji hivyo hivyo kitu ambacho kilikuwa nicha kizamani.

Asanteni.
Naomba kuwasilisha.
🙏
 
Back
Top Bottom