Serikali isaidie kurudisha mali zilizoporwa na viongozi walipokuwa madarakani

Serikali isaidie kurudisha mali zilizoporwa na viongozi walipokuwa madarakani

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
12,675
Reaction score
25,924
Hakuna ubishi kila mtu anajua kilichotokea kipindi cha awamu ya tano kwa vijana wafuatao.

1. Bashite
2. Sabaya
3. Gambo
4. Mnyeti
5. Chalamila na wengine kama kina Ally Hapi though huyo sina uhakika sana.

Wengi waliishi kwa kupora mali za watu. Serikali ikisema itangaze wajitokeze watajaa uwanja. cha kufanya, kwamfano lile la Bashite, kwa nyumba ya mikocheni ni wazi hawawezi kuwa walilipana kwa cash ya mkononi, lazima pesa ni nyingi waliweka bank.

Wamwambie tu Bashite aonyeshe transaction aliyoifanya kudeposit pesa kwa GSM au alete hata wakili au shahidi yeyote kama atajitokeza. wakiona hakuna transaction yeyote aliyoifanya ila analazimisha kwamba amenunua, ni kumrudishia mwenye nayo tu ili haki iwe imetendeka.

Pia watu wenye mali ambazo hawana uwezo kuzielezea, waporwe. kwa RC aliyekaa muda mchache kiasi kile kununua jumba la gorofa Mikocheni, na hana mkopo, hana biashara, sio rahisi. aonyeshe wapi alipata hizo hela. hili lifanyike kwa wale wanyanyasaji wote ili kukomesha lisije kutokea tena mbeleni.
 
kwamfano lile la Bashite, kwa nyumba ya mikocheni ni wazi hawawezi kuwa walilipana kwa cash ya mkononi, lazima pesa ni nyingi waliweka bank. wamwambie tu Bashite aonyeshe transaction aliyoifanya kudeposit pesa kwa GSM au alete hata wakili au shahidi yeyote kama atajitokeza
Kweli watu wanamchokoza Mungu, huyu jamaa asipokujaingiwa kichaa yapo makubwa yatamkuta, si huyu ndiye anasema Mungu amemuinua!!! Kumbe ni mali za unyang'anyi!!!
 
Usisahau tuko kwenye awamu ya nne, matamko mengi bila matendo safari nyingi za nje kusifiana sifiana kwingi

kujipendekeza pendekeza kwingi kuponda yale ya awamu ya tano.

Ya hao watu achana nayo, hakuna kitakachotokea.

labda watakuja tolewa sadaka 2025 kurudisha iman ya watu iliyopotea
 
Kama walioporwa wameridhika sio ubaya. Ila ndio wakati sahihi wa kuwalipizia kisasi Ili iwe funzo kwa wakuja wengine.
 
Lile ford ranger alilompora tajiri wa kampuni ya NAS kwa kumbambika kesi ya madawa bado lipo?
 
Bashite lzm anyolewe denge Hakuna tena Rais msukuma kombe likitoka zanzibar litaenda kaskazini, kisha nyanda za juu.

Wasukuma na kanda ya ziwa watulie kwanza hadi kanda zote ziishe.
 
Huyo DAB msikieni tu, ukipishana naye au ukihusishwa na mtu aliyepishana naye utachagua moja utoe mpunga au uhamishe makazi mkoa mwingine...
 
Wale wote waliopora pesa za wafanyabiashara wa maduka ya kubadili pesa wanafahamika kupitia CCTV. Wafilisiwe warudishe pesa za watu.

Kile kitengo haramu pale cocabs cha uhujumu uchumi kilichoasisiwa na jiwe kimetumika Sana kupora pesa za watz.

Kuna mfanyabiashara wa madini alikuwa na B 25 wakazipora wakamuacha B 3 tu akafa kwa pressure.
 
Kama mtu account yako ilichezewa ndo wakati wa kuishtaki bank nayo bank ikakabane na aliyepora. Maana wabongo walitumia jina la jiwe kuwapiga watz wenzao.
 
Nafikiri wanamwogopa, ana siri nyingi. Akizama yeye atazama na wengi
 
Wale wote waliopora pesa za wafanyabiashara wa maduka ya kubadili pesa wanafahamika kupitia CCTV. Wafilisiwe warudishe pesa za watu.
Kile kitengo haramu pale cocabs cha uhujumu uchumi kilichoasisiwa na jiwe kimetumika Sana kupora pesa za watz.
Kuna mfanyabiashara wa madini alikuwa na B 25 wakazipora wakamuacha B 3 tu akafa kwa pressure.
Habari hii iliwahi kuandikwa wapi mkuu?

Mfanyabiashara huyo anaitwa nani?

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Huyo DAB msikieni tu, ukipishana naye au ukihusishwa na mtu aliyepishana naye utachagua moja utoe mpunga au uhamishe makazi mkoa mwingine...

Kuna video alikuwa anaongea na watendaji wa manispaa, anaongea kwa dharau ya hali ya juu. Kwa kweli alikuwa kenge.
 
Back
Top Bottom