KERO Serikali isikie kilio cha wakulima wa zao la Mahindi wa Nyanda za Juu Kusini

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naomba Serikali isikie kilio chetu sisi wakulima wa zao la Mahindi Nchini hasa nyanda za juu kusini mikoa ya Rukwa, Njombe, Ruvuma.

Bei ya mahindi bado ni ya chini mtaani (350-420)ukiacha bei ambayo Serikali wananunua (700) kwa kilo.

Hoja ni kwamba serikali inanunua Tsh. 700 kilo lakini masharti mengi ya kupokea mzigo wa mteja mfano kulipia usafishaji wa mahindi kwa kila gunia 500, kupakia na kushusha kwa gunia 1000, usafirishaji kupekeka kitengo, Kubwa zaidi pesa hailipwi kwa wakati inaweza chukua mpaka muda wa Mwezi 1-3 kiasi ambacho mkulima mdogo wa tani 1 hatoweza kuendana nayo hivyo kuishia kuuza kwa bei ya hasara kwa wachuuzi mtaani Sh 350-420 kwa kilo ambao ndio hao huenda kupanga foleni kuiuzia serikali.

Biashara ya Mahindi ni huria lakini serikali imedhibiti wanunuzi wengine kutoka nje wasinunue bali inunue yenyewe lakini hakuna uwiano wa bei na wachuuzi wengine wai wameshindwa kudhibiti bei ya soko.

Mkulima wa nchi hii bado ni wa hali ya chini hatoweza kuhimili kumpa mazao serikali na kusubiri kulipwa kwa mda wa unaoweza kufikia mwezi-miezi 3 hivyo anaishia kuuza kwa hasara kwa wafanyabiashara na hao wafanyabiashara ndio wanaenda kuiuzia serikali kwa bei ya 700 kwa kua wanakipato wanaweza kusubiri kulipwa kwa muda huo.

Serikali iwakumbuke wakulima wake na iwasaidie kweli na si kuacha wachuuzi wawaumize wakulima kwa kutoa bei mbaya.

Ushauri
1. Serikali ifanye utafiti wa kina ili kujiridhisha kama kweli mda wanaoanza kununua mazao, hali ya soko, gharama za uzalishaji na bei wanayokuja nayo ni sahihi?

2. Serikali wadhibiti bei ya mazao kwa wachuuzi wengine kama wanavyodhibiti bei za bidhaa zingine kama sukari na kadhalika.

3. Wajadili mbinu itakayo wawezesha kuwahi kununua mahindi tofauti na ilivyo sasa.

4. Wabadilishe mfumo wa malipo eidha walipe kwa hundi mtu akafatikie mwenyewe bank au walipwe cash kwa wale ambao wanadai chini ya milioni 2, ama lah wawaishe malipo isizidi wiki moja (1).

MUHIMU
Kilimo cha zao hili la Mahindi kimebeba watu wengi hivyo basi kupuuza jambo la bei na kuto kusimamia, inapelekea uchumi wa chini na kuendelea kushuka kwa uchumi kwa wananchi walio wengi hivyo kuwa na wakulima Maskini Zaidi na zaidi.
 
na kuendelea kushuka kwa uchumi kwa wananchi walio wengi hivyo kuwa na wakulima Maskini Zaidi na zaidi.
Hifadhi kuna njaa mbeleni, utakuja kunishukuru.
 
Serikali ipi hii yenye kudhulumu wakulima au nyingine. Kulima walime wengine serikali ikuchagulie bei na mnunuzi! How n why?
Tujikomboe kutoka mikono ya watesi hawa Tz itakuwa na maendeleo sana. Lakini kama ni hii awamu ya ngapi vile mnajidanganya sanaaa
 
Back
Top Bottom