Serikali isimamishe shughuli za Precision Air haraka

Serikali isimamishe shughuli za Precision Air haraka

Yaa, nafikiri hili na lenyewe lilikuwa tatizo, ilikuwaje cabin crew hawakufanya jitihada za ku evacuate abiria, badala yake nimesikia wao waliruka kujiokoa. Otherwise, they were taken at a surprise........hawakuwa na idea ni kitu gani kilikuwa kinaendelea.
Actions speaks louder than words, kwa kuangalia zile clips za uokoaji unapata picha cabin crew awakujua nini chakufanya.

Ata ukisikiliza abiria waliopona mmoja anasimulia maji mpaka yameanza kuwafika mabegani ndio cabin crew mmoja akakumbuka kufungua emergency door.

Milango ya ndege za abiria ina sliding floaters for emergency use unapofungua floaters kwenye maji ndege inakuwa na muda wa kuelea, kuweza kutoa watu wote, hakuna abiria alievaa life jacket na kutolewa kwa life raft ya kuwawekea watu wakati wanasubiri kuokolewa.

Tatizo kubwa hapo ni precision air had they deployed emergency evacuation procedures kusingekuwa na vifo; wavuvi wamefika ndege aija-jaa maji ila milango bado aijafunguliwa.

Lawama number moja kwa watu waliesababisha vifo vinavyoepukika ni Precision Air.
 
Nakubaliani kuwa ile Route ya Mwanza to Bukoba ni hectic one. Mwaka fulani nilipita ile distance ya Mwanza to Bukoba dakika 5 niliziona ni kama Miaka 100.

Ni kama ndege ilikuwa inavutwa kwa lazima back and forth... kibaya zaidi Rubani hakutangaza chochote.

Ni siku ambayo nilisikia Yesu akitajwa zaidi kuliko siku yoyote. Wapo waliozimia kwa Hali ile.

Mimi na Mzungu tulikuwa tumechili.... ndani ya nafsi yangu nikajisemea. Kama leo ndio mwisho wangu .... let the shit happen .... I can’t deny death . Only to realize that I was born to die.

So nikawasha ipad yangu na kuanza kusikiliza the Beatles, waiting for my destiny.

I was eager to see my new beginnings.

Well , baadae ndege ikatua and from that moment nikasema hii ruti sipiti tena. Ikiwa nina Safari ya Bukoba... nina segment safari kwa Lami kwa siku 2.

Ile Distance Mwanza to Bukoba kupitia ziwa , There must be something wrong apart from Nguvu ya Mvutano.

Hoja yangu ya Msingi ni kuhusu hizi ndege za Precision

Mwaka 2011, pale KIA nikiwa na Lowasa na Sumaye, Tairi ya Precision ilipasuka wakati wa kutua , kukatokea taharuki kidogo lakini tukatoka salama.

2018 pale Tabora, tulitumia 30 minutes kutua kwa sababu tairi za ndege zilikataa kuchomoka, kila jamaa akijaribu tairi hazitoki.... baadae tukatua , Jamaa wakadai kuwa ni kawaida kwenye ndege.

Mwaka 2021, Hapo ndio nikaanza kuwaza kuhusu Precision, pale JNIA, tulitua kwa vibaya snaa kana kwamba tupo vitani.

Nimepanda ndege nyingi But ule mtuo, kila mtu alistuka na tukauliza nini shida... hawakutoa majibu.

Hapo hapo JNIA siku nyingine , wakati wa kutua , tairi ni kama iliwaka moto yaani ile kutoa cheche nyingi .... na ilipotua ilitua kwa kishindo ambacho sio cha Kawaida na kila mtu alihoji na wote tulistuka sana.

Baada ya hapo nikawa nimeona Red light , nikasema sipandi tena hizi ndege za Precision

. Majibu yao baada ya kuhoji yalikuwa ni Joto la Dar ni kubwa ndio maana tairi zimewaka moto.

Inawezekana kabisa hali ya hewa ilichangia kutokea ajali lakini Inawezekana kwa asilimia kubwa ndege ilikuwa na shida kama kawaida yao.

Rubaga ni Rubani wa zaidi ya Miaka 25 kwenye kazi hiyo , anajua well enough nini cha kufanya kwenye mazingira hayo ya hali ya hewa...alikuwa anaweza kurudi Mwanza na ni mara nyingi alishafanya Hivyo.

Ile ya juzi, ni tatizo la ndege ilipoteza control na ikagoma kutua kwa kutokana na hitilafu ndani ya mfumo wa matairi na mfumo wa injini. Ukijumlisha na hali ya hewa , mambo yakaharibika zaidi.

Naishauri Serikali, Isimamishe shughuli zote za Precision na kufanya uchunguzi yakinifu.

Kufanya special inspection ya ndege zote zinazomilikiwa na Precision Air ikiwa ni pamoja na kufanya “Age analysis”. Usikute haya mandege yamesha Expiry muda wake wa matumizi.

Kufanya special inspection kwa injinia wote wa Precision wanaokagua ndege kabla na baada kama kweli wana vigezo.

Mkurugenzi wa Precision awekwe chini ya ulinzi to extend further special inspection..... machozi yake yana maana nyuma ya pazia , wanajua wazi kuwa hawalipi vyema mainjinia wa Technical inspection. Matokeo yake wanafanya kazi les affairs na kisela.

Wanakagua ndege na kuzibaziba pancha kama waziba daladala za Buza.

Hali ya hewa inachukua nafasi ndogo sana kwenye ile ajali, ile ndege ilikuwa ni MBOVU.

Rubani aliyeendesha ni Experienced one , kwa hali ya hewa alikuwa na option nyingi na kwa kufanya mawasiliano na watu wa nchi kavu angeenda kutua Mwanza.

Hapo chini ni uzoefu wa Rubaga... ni zaidi ya 30 years

Captain Buruhani Rubaga

Captain

Precision Air Services PLC
2003 - Present · 19 yrs 11

Zantas Air
1993 - May 2003 · 10 yrs 5 mos

First Officer
AIR TANZANIA COMPANY LIMITED
1990 - 1993 · 3 yrs Bachelor's degree, Mechanical Engineering
1983 - 1987 Sri Jayachamarajendra College of Engineering, Mysore (QIP Centre)

Serikali TAKE Action au Mtazika watanzania wengi
Naanza kuamini kuna namna ya vita ya kibiashara juu ya hili 🤔🤔🤔
 
Badala iongee wizara ya uchukuzi, shirika la usafiri wa anga tz , ana ongea msemaji wa serikali Ambae kitaaluma NI jonalist, Ila amesema black box imeonekana,
Na vyombo vya usalama wa anga from foreign countries,vimekuja kufanya uchunguzi.
Tuna taka serikali yetu isiingilie huu uchunguzi, iache mamlaka ifanye KAZ yake
 
Kila mtu humu mtaalamu, Hadi raha
Unaishi zama za age of information and information is power. Ukiingia youtube kuna academics wanafundisha ‘special relatively’ from scratch na hesabu zake ushindwe wewe tu kuelewa if understanding astrophysics is your thing.

Kama hujui hesabu huko huko YouTube kuna watu wanakupa route yote ya modules muhimu zote hadi kuwa mathetacian, na vitabu vya kununua from elementary mpaka final degrees. Better still kuna lecturers kibao wakukufundisha kila module utakayoamua kuisoma na ukiona lecture mmoja umuelewi kuna zaidi ya kumi wengine ni wewe kuchagua yupi Mwalimu mzuri.

Sasa itakuwa hizo videos za emergency training kweli za ndege sio tu kwamba kuna video za mashirika mbali mbali za training, bali na video za ajali zenyewe chungu mzima. Kuna video za ndege luluki ambazo engine zinawaka moto zinakimbilia kutua majini na watu wote wanatoka salama; mara zote wanaofika wa kwanza ni civilians.

Dunia ya leo kukubali kulishwa mawazo ya watu wengine kwa tafsiri yangu ni uvivu wa kujifunza tu au kushinda kusikiliza habari za ujinga mitandaoni sijui mpuuzi gani kafanya nini.
 
Hali ya hewa inachukua nafasi ndogo sana kwenye ile ajali, ile ndege ilikuwa ni MBOVU
Kwa hiyo, tume ya uchunguzi tuifute na tufanye maamuzi kupitia ripoti yako hii?

Waswahili tuna shida gani jamani? Shusha adrenaline yako kwanza ili upate nafasi nzuri ya kudadavua mambo. Ni hilo tu nakuomba ufanye!!!
 
Kwa hiyo, tume ya uchunguzi tuifute na tufanye maamuzi kupitia ripoti yako hii?

Waswahili tuna shida gani jamani? Shusha adrenaline yako kwanza ili upate nafasi nzuri ya kudadavua mambo. Ni hilo tu nakuomba ufanye!!!
tume ya nini wakati kila kitu kipo wazi.
 
camera kwenye nyumba ya Lissu hadi wa leo hazijaonekanaga itakuwa hiyo black box ? huijui bongo wewe.
Sio camera tu hadi dereva leo hii hajulikani yupo wapi. Tupo sawa hapo?
 
Sio camera tu hadi dereva leo hii hajulikani yupo wapi. Tupo sawa hapo?
yeah, hadi dereva atakapopatikana ndiyo uchunguzi utaanza, kama hatapatikana basi na uchunguzi wa tukio zima haupo kwa mujibu wa Police Bongo movie sababu Dereva ana nyaraka zote za kesi.
 
Kuna mwamba mmoja ni mchaga amesomea mambo ya uhasibu alipata kazi kwenye hili shirika miaka kama 7 hivi iliyopita.
Ghafla jamaa akawa tajiri na kazi akaacha, ila za chini ya kapeti inasekana jamaa na wenzake kama 3 walipita na milioni kama 400 za shirika!
 
Sasa matatizo uliyotaja hayapo kwenye airlines nyingine?
Alafu mental maturity is very subjective labda kama ungekuwa na approved testing kits

Yapo wapi ?

Subjective is overstatement , pole
 
Uchunguzi ni muhimu sana, ila shida huwa inakuwa kwenye matokeo ya uchunguzi, yakuwa yamejaa siasa kuliko utaalamu na hivyo kupindisha ukweli. Pia tukumbuke kuna maslahi ya watu kwenye hii biashara.

Umeongea vizuri
 
Back
Top Bottom