SoC04 Serikali isisubiri matukio ndio itoe ajira

SoC04 Serikali isisubiri matukio ndio itoe ajira

Tanzania Tuitakayo competition threads

Mkola Tz

Member
Joined
Sep 10, 2021
Posts
18
Reaction score
15
SERIKALI ISISUBIRI MATUKIO NDIO ITOE AJIRA

Serikali yetu imekuwa itumia ajira kutuliza matukio ya kisiasa, kiuchumi, au majanga yanayotokea hapa nchini. Ili kuwa na utawala bora Kuna haja ya kuwa na mipango mizuri katika utoaji wa ajira hizi kwa vijana wa nchi hii, leo hii ajira ndio zimekuwa zikitumika kutuliza mambo ndani ya nchi. Yaani ikitokea watu wanadai katiba mpya, vikao vya bunge ambavyo huzua taharuki kwa wananchi na mifumuko ya bei za vitu hapa nchini, ajira ndio zinakuwa kitulizo cha mada hizo.

Ukifuatlia kwa umakini utagundua kumekuwa na tabia ucheleweshaji wa utoaji wa ajira hapa nchini na si kwa sababu za msingi bali uendane na hali ya nchi itakavyokuwa. Mfano Rais anasaini kibali cha ajira na watangaza kupitia wizara husika lakini utokaji wake ndio unakuwa shughuli mpaka Jambo baya liikute inchi iwe mafumuko wa bei, ajali au mitafaruku ya bungeni Sasa hapo ndio serikali huamua kuachia ajira ili kupotezea na kupoza tukio hilo.

Inakuwaje taifa linakuwa halina mipango sahihi ya utoaji ajira mpaka wawe wanasubiri tatizo litokee ndio watoe ajira, hapo ni sawa kutupiga na kitu kizito kichwani tutakuwaje na utawala bora ndani ya nchi wakati tunasubiri sababu au tukio ili tuachie ajira hizo, hapo hakuna cha maana zaidi ya kuwazubaisha wananchi tu na kuwatoa katika katika mstari/msimamo wao juu ya jambo fulani ndani ya nchi.

Serikali imetangaza ajira mpya mwaka huu 2024 lakini hamna taarifa yoyote ile kwamba zitatoa lini ajira hizo, zaidi ya kusubili tukio lolote litakalojitokeza ndani ya nchi alafu ndio watoe ajira hizo ili kupoza wananchi kulizungumzia hilo tukio, hivyo inawabidi watoe ajira na watu wasahau kuhusu tukio au tatizo linaloikabili nchi na kubaki kuzungumzia ajira hizo tu. Kutumia kwao mifumo huo ni moja kigezo cha kutokua na utawala bora ndani ya nchi.

Mipango Kama hiyo haileti utawala bora nchini, bali uzugaji kwa wananchi na utoaji wa ajira hizo unatumika vibaya kwani ni kama suluhu ya watawala katika kukamilisha mipango yao hapa nchini. Wananchi wanakuja kukaa sawa na tukio hilo wanakuwa wamesha chelewa na kuvurugwa na ajira hizo.

Miaka ya uchaguzi pia ajira zimekuwa zikituma kwa kampeni za viongozi, wimbo unakua ni ajira kwa vijana tu sasa utashangaa kuona kila wizara zinaanza kutangaza ajira hizo. Kitu ambacho unabaki nacho kichwani ni kwamba hizi ajira zinakuwaga wapi? Kipindi chote hicho. Serikali inawezaje kutoa kibali afu ikae kimya kiasi ndio unagundua kuwa wanasubiri kipindi kama hichi cha uchaguzi kwa maslahi yao binafsi. Hatuwezi kuwa na utawala bora kama tutakuwa tunasubiri misimu ya uchaguzi ndio tutangaze ajira nyingi kwa vijana.

NINI KIFANYIKE ILI KUONDOKANA NA TATIZO HILI
Serikali inatakiwa kuwa na muda maalumu wa utoaji ajira ndani ya mwaka wa bajeti husika kama ni mwezi wa sita (6) tu na si kusubiri waone kuna tukio au tatizo gani lililo jitokeza. Hiyo itapunguza shida ya namna hiyo na ndio utakuwa uhimizaji wa utawala bora ndani ya nchi kwani hakutakuwa na nafasi ya wao kusubiri kuna nini au tukio gani nchini ndio waachie ajira.

Tusisubiri wakati wa uchaguzi ndio tuachie ajira nyingi, serikali na taasisi zingine zisisubiri kipindi cha uchaguzi ndio zianze kuachia ajira ambazo nyakati zingine zimekua shida kwa wananchi kuzipata. Tutakuwaje na utawala bora wakati tunasubiri misimu ya kampeni kuachia ajira hizo, pia inakuwa na manufaa kwa viongozi walio madarakani kwani wanakuwa wanakitumia kama kigezo chao wao kurudi katika nyazifa zao.

Kuna haja ya watu kulipigia kelele suala hili mpaka serikali iliwekee utaratibu ulio sahihi kwani bila kulizingumzia na kulipazia sauti hali itabaki kuwa hivi ili ajira ziwe zinapatikana kwa wakati Ni kuwe na uchaguzi au ndio Kama hivyo kuwe na tukio ambalo linaikabili serikali yetu na nchi kwa ujumla, kufanya hivyo kutachangia kusukuma watu walio madarakani au wahusika wa utoaji kazi hizi kukumbuka wajibu wao. Kufanya hivi itapelekea utawala bora.

HITIMISHO
Kuja haja kama taifa kuwa na sera madhubuti kwenye masuala ajira kwani hurudisha matumaini kwa wananchi wengi. Hivyo basi ajira zisitumike kama chanzo cha kutuliza mambo ndani ya nchi kufanya hivyo kutahimiza utawala bora wa serikali yetu. Serikali iweke utaratibu sahihi wa muda na si kusubiri jambo fulani wala nyakati za uchaguzi ndio ajira zitoke kwa usahihi, kutangaza ajira mapema baada ya rais kutoa kibali cha ajira kutahimiza utawala bora ndani ya nchi. Viongozi walio madarakani wasitumie njia hii kujinufaisha wao katika kipindi chao cha uongozi, kwani tatizo linapotokea na mkasubiri mtoe ajira ili kupoza raia huko ni kujinufaisha wao wenyewe, na hapo ndio unakosekana utawala bora, ili uwe bora inakupasa kutoa taarifa hizi kwa wakati sahihi.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom