Serikali Isitishe Mauaji na Uporaji wa Ardhi Katika Kijiji cha Kalilani - Kigoma

Serikali Isitishe Mauaji na Uporaji wa Ardhi Katika Kijiji cha Kalilani - Kigoma

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
643
Reaction score
1,603
act w.jpg
act w1.jpg

Chama cha ACT Wazalendo tunalaani vikali vitendo vya kinyama vya mauaji, uharibifu wa mali, ukiukwaji wa binadamu katika operesheni za kuwaondoa wananchi kwa nguvu kwenye ardhi zao nchini. Tumesikitishwa sana na tukio la hivi karibuni katika Kijiji cha Kalilani, Kigoma la Seikali kupanga kuvifuta vitongoji vya Mahasa na Kabukuyungu huku likisababisha maumivu makali kwa wananchi ili kupanua Hifadhi ya Taifa ya Mahale.

Serikali kwa kushirikiana na Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale, imeendesha operesheni za kijeshi tangu mwaka 2023 kwa lengo la kuwaondoa wananchi wa vitongoji vya Mahasa na Kabukuyungu. Operesheni hizi zimepelekea kupoteza maisha ya watu watatu: Fedhali Kalabula, Warutundu Kasimu (2023), na Omari Yusufu (2024). Wananchi hawa wamepoteza makazi yao, huku taasisi za elimu, afya, na dini zikiwa hatarini kubomolewa.

Madai ya Serikali kuwa wananchi wa Kalilani wanaishi kwenye eneo la hifadhi ni uwongo mtupu na yanaonyesha njama za kupora ardhi yao. Kijiji cha Kalilani ni kijiji halali kilichosajiliwa Juni 15, 1995 kwa namba KGM-182-09003026, kikiwa na vitongoji vinne: Kabukuyungu, Kalolwa, Katumba na Mahasa. Serikali inashindwa kueleza ni kwa nini sasa inataka kuwaondoa wananchi ambao wameishi hapo kihalali kwa miongo kadhaa.

Vilevile, madai ya kwamba fidia imeshatolewa kwa wakazi wa vitongoji vya Mahasa na Kabukuyungu sio kweli. Fedha zilizodaiwa kutolewa Shilingi Bilioni 1.68 – hazijawafikia wananchi waliostahili, zimeliwa na wajanja wachache. Aidha, Serikali inasema uongo kwamba mgogoro umeisha, wakati ikitoa tangazo la kuwaondoa wananchi ifikapo Machi 25, 2025. Hii ni ishara dhahiri ya unafiki na ukandamizaji.
WhatsApp Image 2025-03-21 at 15.27.33_67a8005a.jpg


Video kutoka Maktaba ya kilichotokea katika Vijiji hivyo
​
Serikali imeonyesha kutojali vilio vya wananchi. Wiki mbili zilizopita, ACT Wazalendo ilitoa tamko la kutaka uwajibikaji kutokana na mauaji ya raia katika Wilaya ya Kisarawe, Pwani, pamoja na kuondolewa kwa nguvu kwa wananchi huko Ilijia, Ilamba, Morogoro na Kilindi. Mpaka sasa hakuna aliyewajibishwa. Waziri wa Maliasili na Utalii anaendelea kutamba kana kwamba mauaji haya ni jambo dogo.

Ni wazi kuwa, kama hatua hazitachukuliwa sasa, tutaendelea kushuhudia vitendo hivi vikiendelea katika maeneo mengine. Hivyo, ACT Wazalendo tunatoa wito kwa serikali

i. Kusitisha mara moja operesheni zote za kuwaondoa wananchi katika Kalilani na maeneo mengine.
ii. Kufanya uchunguzi huru kuhusu mauaji, uporaji wa ardhi, na uharibifu wa mali.
iii. Kuawajibisha wahusika wote wa vitendo hivi vya kinyama.
iv. Kuweka wazi mpango wa matumizi ya ardhi na kuhakikisha wananchi wanashirikishwa.

Serikali ya Rais Samia imeonyesha wazi kabisa kupora haki za wananchi wanyonge na kutoguswa na vilio vyao. Tunamtaka Rais Samia Suluhu kumwajibisha Waziri wa Maliasili na Utalii kwa kushindwa kusimamia haki za wananchi.

Pia tunasisitiza kuundwa kwa tume maalum ya kijamii ili kuhakiki mipaka na matumizi ya ardhi kwa haki na uwazi.

Imetolewa na;

Ndg. Juliana Donald Mwakangw`ali
Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii
ACT Wazalendo
21 Machi 2025
​
 
Aiseee kuna wale Jamaa pia .....au basi ila ilikua Kigoma pia pale Uvinza kwa juu kuelekea Kasulu.
 
Back
Top Bottom