Serikali itamke umri wa binti kufanya kazi za ndani uanzie miaka 18

Serikali itamke umri wa binti kufanya kazi za ndani uanzie miaka 18

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251

Naiomba Serikali ya Tanzania na ofisi za haki za binadamu kuwe na umri sahihi wa kumwajiri mfanyakazi wa ndani. Kama ilivyokuwa na umri sahihi wa kupiga kura kuanzia miaka 18, basi kuwe na umri sahihi wa kumwajiri mfanyakazi wa ndani.

Cha pili, mfanyakazi wa ndani awe na kibali cha kuruhusiwa kufanya hiyo kazi. Cha tatu, asiwe amekatishwa masomo yake kwa sababu gani? Unakuta mtoto ni mdogo amefaulu kwenda sekondari lakini wazazi wake wanampeleka kwenda kufanya kazi za ndani—umeelewa? Alafu wanatumumiwa wao pesa, sindio?

Akifika kwenye kufanya kazi za ndani anakutana na mambo kama hayo, anapata magonjwa, anabakwa, anabebeshwa mimba, yaani anateseka kikatili, inafikia hatua mpaka unakuta anachomwa na pasi! Hivi mtoto wa miaka 10 unakuta anapika chakula cha nyumba nzima ya watu labda saba, nane; hiyo inakuingia kweli akilini?

Kwa hiyo, mimi naiomba Serikali, yaani watu kuwe na umri sahihi kabisa kwamba huyu anatakiwa kufanya kazi za ndani ana umri huu, na kuwe na kibali kabisa kinachoruhusu huyu kufanya hii kazi."
 
Unawajua wabeki tatu? Au unawasikia..wakianza kupendeza wanamzidi hata mama mwenye nyumba..unategemea baba mwenye nyumba au watoto wake wataacha kumtafuna na kumjaza upepo.
 
Wahuni hua wana akili sana pia wana huruma,
Ugomvi wao na Mungu ni kutokwenda kwenye ibada tu,

Kijana kanyooka hadi kanyooka tena.
 
Back
Top Bottom