Serikali itangaze tarehe ya kuwarejesha vyura wa Kihansi ili wadau wa mazingira tukawapokee uwanja wa ndege

Serikali itangaze tarehe ya kuwarejesha vyura wa Kihansi ili wadau wa mazingira tukawapokee uwanja wa ndege

Kwa taarifa tu ni kwamba vyura 100 wa Kihansi wa kwanza kurudi kutoka USA ilikuwa ni mwaka 2010.

Walitua nchini kwa KLM na walipata hadhi ya first class. Pilot na crew walifanya special program kwenye ndege yao na walifanya competition kwa watoto wachore picha ya vyura wakirudi nyumbani (picha zilikuwepo). Hata wao wenyewe walipiga picha na vyura hao. Walifikia kwenye captive breeding facility UDSM.

Vedasto Msungu (RIP tunakukumbuka mwanamazingira mahiri) aliripoti ujio wa vyura hawa kwenye vyombo vya habari.

Tarehe 31 October, 2012 batch ya kwanza ya vyura hawa walipelekwa mlimani kwenye makazi yao ya asili (reintroduced). Lilikuwa ni tukio la kimataifa na wanasayansi wengi wa kitaifa na kimataifa walikuwepo (WCS, IUCN, UDSM, SUA...) na liliripotiwa na vyombo vya kimataifa.

Vedasto Msungu na team yake walikuwepo na waliliripoti hili kwenye vyombo vya habari.

Shida yetu sisi waTz huwa hatuna habari na mambo ya mazingira na wala hayatuhusu, kazi yetu ni kulalamika tu.
Weka video tuone
 
Nimekwambia mwaka 2010 enzi zile bado smartphones zilikuwa kidogo sana.

Vedasto Msungu ndiyo alikuwa mtoa ripoti yeye alikuwa na mwenzake akichukua video.

Ukiniambia mimi utakuwa unanionea bure.
Basi sikuonei tena.
Ila umeshawahi kukisoma kitabu cha Eat that Frog?
 
Kwa muda wote waliokaa marekani kila chura atakuwa na mizigo mingi labda serikali iwakodie lile dege la mizigo lililotua KIA
 
Back
Top Bottom