raiamwematz24
Member
- Dec 6, 2025
- 8
- 21
Vurugu zilizotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 29, 2025 zimeacha alama nzito ikiwa pamoja na kuchafua diplomasia na uhusiano wa kimataifa.
Vurugu hizo zilizotokana na maandaano katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Kilimanjaro na Njombe, zimesababisha mauaji, majeruhi na uharibifu wa mali.
Akizungumzia athari za vurugu hizo, mchambuzi wa masuala ya diplomasia Kelvin Msemo (Si jina lake halisi, hakutaka kutumia jina lake kwa sababu binafsi) amesema ni wazi kwamba uhusiano wa kimataifa kati ya Tanzania na nchi nyingine hasa zilizoendelea utatetereka, akisisitiza kwa sasa Tanzania inapaswa kuboresha misingi yake kidemokrasia na uchumi.
“Ukishachukiwa na Marekani ni ngumu Ulaya akakupenda,” amesema.
Amesema hatua ya nchi ya Marekani kutoteua balozi nchini Tanzania na kubakia na kaimu balozi tu, ni ishara mbaya katika uhusiano wa kimataifa.
Tayari Marekani imeshaeleza kutoridhishwa na yaliyotokea katika uchaguzi mkuu na kusema wanatafakari uhusiano kati yao na Tanzania.
Amesema kuwa mataifa makubwa kama Marekani yanahitaji nchi ambazo zinahitaji kuwapa vipaumbele kwenye sekta za uwekezaji na maeneo mengine.
“Ukiangalia sasa kwa mfano bandari wanaoendesha ni DP World ambao ni Waarabu, ukija upande wa TAZARA (Mamlaka ya Reli kati ya Tanzania na Zambia), sehemu kubwa wanasimamia Wachina, hiyo pia sio jambo la kuridhisha kwa Marekani,” anasema.
Pia soma ~ Papa akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania
Anaeleza kuwa kilichotokea kuanzia Oktoba 29, 2025 kimeacha makundi mengi ndani na naje ya nchi, hivyo lazima kidiplomasia hali haitakuwa na utulivu kama ilivyokuwa awali.
Licha ya tangazo hilo, Serikali ya Tanzania ilijibu kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Thabit Kombo akisema kuwa Tanzania haitakabiliwa na njaa wala kusimama kwa maendeleo licha ya Umoja wa Ulaya kusitisha misaada, kwani ina vyanzo vingi vya mapato.
Kenethy Marcel, ambaye ni mchambuzi wa masuala ya diplomasia anaeleza licha ya matukio ya uchaguzi, ni kwa muda sasa serikali iliendelea kuijenga diplomasia yake kimataifa kupitia ziara za viongozi wa serikali nje ya nchi na hata ushiriki wa mikutano.
‘‘Tanzania bado ni kisiwa cha amani, ingawa wapo wanaojenga hoja za kutaka kuiharibu,’’ amesema.
Amesishauri Serikali kuwasikiliza walioandamana na kutoa suluhu, nginevyo kutakuwa na mpasuko kati ya wananchi na serikali.
“Nchi inaposhindwa kudhibiti mivutano ya kisiasa, inakuwa rahisi kwa mataifa mengine kuingilia kwa kauli, shinikizo au hata sera,” anasema mchambuzi mmoja wa siasa za kimataifa aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina.
Huyu anasema mahali popote panapokuwa na vurugu, hakuwezi kuwa na siasa nzuri, ukiukwaji wa haki huongezeka na hata misingi ya demokrasia huvunjwa.
Novemba 27, 2025, Bunge la Ulaya lilipitisha azimio la kuitaka Kamisheni ya Umoja wa Ulaya (EU) kusitisha mpango wa ufadhili kwa Tanzania baada ya ghasia za uchaguzi kusababisha mauaji ya raia na uharibifu wa mali katika miji mbalimbali nchini.
Hata hivyo, ripoti za vyombo vya habari za kimataifa ikiwemo BBC zilieleza kuwa jukumu kuu la kusitisha ama kuendelea kuifadhili Tanzania lipo mikononi mwa kamisheni hiyo ya Umoja wa Ulaya.
Kwa mujibu wa Mwanadiplomasia Mbunda, kupitia taarifa iliyochapishwa na DW Kiswahili “Nchi zilizoendelea kama za Ulaya hazisaidii nchi zinazoendelea kwa maana ya kutoa misaada tu, nchi zilizoendelea zinahitaji vilevile mikopo ya masharti nafuu, nchi hizo zinahitaji hadi mikopo ya bei nafuu kwa benki kubwa, ambazo wahisani wakubwa wa benki hizo au wenye hisa wakubwa wa benki hizo ni nchi hizo hizo za magharibi."
Pamoja na mijadala kuwa mingi kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii, Serikali ya Tanzania imeendelea kuimarisha uhusiano wake kupitia ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo.
Alikutana na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Wawakilishi la Marekani ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Florida kutoka Chama cha Republican, Brian Mast na kukubaliana kuimarisha na kukuza ushirikiano na uhusiano wa kidiplomasia kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Marekani.
Lakini hili pia lilidhihirika mapema baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kukutana na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Andrew Lentz, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma, miongoni mwa yaliyojadiliwa ilikuwa ni kukuza maeneo ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Mgogoro wa Kidiplomasia ni mtihani mkubwa kwa historia ya nchi yoyote ikiwa hakutakuwa na misingi ya kujiimarisha kiuchumi na kiusalama zaidi.
Hatima ya Tanzania katika mwelekeo wa kimataifa itategemea uwezo wake wa kusawazisha maslahi ya ndani na matarajio ya jumuiya ya kimataifa, Diplomasia ya busara, inayojengwa juu ya ukweli, mazungumzo na mageuzi ya ndani.