Serikali itatue kero za walimu ili BRN Ifanikiwe

Serikali itatue kero za walimu ili BRN Ifanikiwe

NJALI

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2014
Posts
1,534
Reaction score
1,090
Serikali yetu ni sikivu japo kusikia kwake huwa ni kwa msimu na husikia sikio moja. Walimu tunaishi maisha magumu, mshahara kiduchu, nyumba za walimu hakuna! Mwalimu anatakiwa akapange chumba japo kimoja kwa maana fupi tunaishi stoo, kodi ya nyumba ni mshahara huo huo kiduchu. Pia vyumba vya madarasa vichache hivyo msongamano unakuwa mkubwa kwa darasa. Mfano shule niliopo darasani form three wako mikondo 3 kila mmoja una wanafunzi 88! Je ni sawa? Pia kuwe na allowances za kusahihisha, kupanga matokeo na ualimu wa zamu maana ni tofauti na kufundisha. Mbona wabunge wanamifuko ya jimbo? Mbona wana sitting allowance na seminars pia vikao vya kamati? Why not to teachers and other sectors. Sijui kama BRN inawezakufanikiwa bila kujali maslahi ya walimu.
 
Poleni sana walimu,
Tatizo lenu ushirikiano F...
Naamini siku mkiungana kwa pamoja mambo yatakaa sawa..
 
Walimu hatuna ushirikiano kwa kuwa hatuna chombo mahususi cha kutetea maslahi yetu. Chama cha walimu kinahujumu walimu, sina hakika kama vigogo wa CWT wana nia ya dhati ya kumsaidia mwalimu kama wanavyo toa macho kukata 2% kwenye mishahara yetu. Bora waachie ngazi kama wameshindwa kazi.
 
Back
Top Bottom