Suala la ajira ni wakat wa serikali kuangalia mfumo wa kielemu mahitaji yetu kwa sasa ni tofauti na kipindi tunapata uhuru Tanzania kipindi cha uhuru tulikuwa tunaitaji wasomi ila sasa sidhani kama mahitaji ya wasomi ni makubwa sana.
Wasomi wapo wengi sana ni wakati sasa wa kudeal na kuwekeza kwenye fani ambazo huitaji kuajiriwa unaweza kufanya mwenyewe mfano ufundi tuboreshe Veta na vyuo vya ufundi ikibidi hata tutoe na mikopo kuwa shawishi watu kwenda kusomea ufundi huyu fundi ni vyepesi kukulipa mkopo kwa maana akimaliza tu anaweza kujiajiri na kuanza kutengeneza pesa kuliko huyu uhasibu, Doctor, Engineer ambae mpk apate ajira ambazo hazipo.
Kipindi tunaitaji wasomi tuliwekeza nguvu kubwa mpaka kila mtanzania akaamini degree ndo kila kitu hii ikapelekea kupatikana mpk Degree za Chupi na watu kuanza kufoji vyeti imefikia hatua tofauti ya msomi na darasa la saba kuwa ni cheti tu.
Hatuwezi kuendelea kwa kutengeneza taifa la white collar jobs sasa ni wakati wa kutengeneza blue collar jobs pia kudhibiti idadi ya wanaoenda vyuo waende wale wenye sifa kweli kweli mfano hata kwa mwaka tukizalisha wasomi laki 2 mwenye weledi inatosha kuliko kuzalisha wasomi laki 8 ambao hawana tija zaidi ya mavyeti tu
Waende vyuo wachache wengi waende Veta na vyuo vya ufundi na wapate mikopo kabisa kama hawa wanaoenda vyuo
Tusiizingizie elimu, swala la ajira limetengenezwa na mifumo ya dunia Kwa sababu maalumu Africa ikiwemo kuwatumia vijana ku destabilize serikali zitakazokaidi maelekezo yale ya jumla ya wenye nguvu za kiuchumi...
Hakuna shida ya kuajiri Tanzania na elimu hii ni sahihi kwakua duniani kote wasomi wa Tanzania wana fit wanapoendelea na masomo yao kwenye vyuo vingine nje ya nchi; ila imekosa sehemu ya kufanyiwa mazoezi ya ukweli ambayo ndiyo hiyo ajira na hivyo kuna mismatch kati ya matumizi ya rasilimali watu na kazi wazifanyazo, hivyo hao wasomi kushindwa kuwa mahiri katika nyanja zao. Hii inaongeza umasikini na pia kusababisha nchi kushindwa kujitegemea. Ikitokea hivyo tunaendelea kuwa tegemezi na nchi zetu zinaendelea kutotumia rasilimali zake inclusing watu, hivyo kuwawezesha hayo mataifa kuendelea kuzitumia kwaajili ya viwanda na matumizi yao mengine. Hii pia huwapa nafasi ya kuendelea kutawala masoko na kuendelea kuwa mataifa yenye nguvu duniani.
Pamoja na hayo yote, bado kuna sababu za msingi mataifa hayo kufanya hivyo na hata tukikubali kuwa kama wao watakavyo bado hali ingekuwa afadhali kama wachumi wetu wangeondoka katika kulazimisha model zile za darasani ambazo hazi fit vizuri kwenye nchi zetu kwasababu hizo hizo nilizotaja hapo juu kwakua uchumi wetu bado haujafikia kiwango cha soko i.e market economy ambapo sasa model hizo zingeweza kufaa.
Kilimo kwamfano, ni sehemu ambayo inaweza kuajiri vijana karibu wote wasomi wa Tanzania na kikizingatiwa katika context yake kingeweza bado kuelekeana na hiyo mifumo ya kiuchumi ya dunia pasipo misuguamo mikubwa na kwakutumia negotiation na diplomacy za kibiashara. Lakini nimesikitishwa kidogo juzi na maelezo ya Waziri wa kilimo kwamba wanadhamiria kununua piki piki kwa wagani ili wawatembelee wakulima...Japo bado ni mwanzoni, lakini naona failure kabla ya kufikia mwisho na kuona outcome. Hii ni kwakua mbinu hii imepitwa na wakati na ni mzigo mno kwa taifa ukiangalia pesa ambazo zitahitajika na kiwango cha uwezo wa mkulima huyo anayemlenga kumpa huduma hiyo kuongeza tija...We fikiria huyo mgani ambaye siyo sehemu ya uzalishaji wa moja kwa moja umlipe mshahara na marupu rupu yake, umwekee mafuta ya pikipiki akatembelee wakulima let say 30 au hamsini kwa siku atatumia muda gani kutoa elimu gani ambayo huyo mkulima pamoja na level yake ya elimu na vipingamizi vingi alivyonavyo including household labour ambayo wengi ndiyo hao wamekimbilia mijini na hawana ajira, kuongeza tija?
Hizo bilioni zitapotea jinsi ile ile hizo bilioni za mikopo kwa vijana na wanawake zinavyopotea kwakua zinasambazwa kwa watu wengi wasio na uwezo wa kuongeza tija.
Pesa hizo zikitumiwa kwa jinsi nyingine ambayo hapa siwezi kueleza kwasababu maalumu zitaweza kuajiri hao vijana wote waliosoma na wasio soma kisha wakaongeza tija na kutengeneza uchumi ulio imara na wenye uhakika wa soko la ndani...
Muundo ninaouwaza utawavuta vijana wa mjini kurudi vijijini kupata ajira na hiyo mikopo itafaa kuchochea uchumi tofauti na sasa ambapo unatumiwa kuwa madalali wa bidhaa za china, hivyo kutengeneza uchumi wa china zaidi kuliko ule ya Tanzania na Africa.
Mh. Mama Samia ni msikivu, mtulivu, kwa mara hii ninamatumaini atawasikiliza wataalamu wa Tanzania si kisiasa wala si kwakuwapa vyeo bali kuwa integrate kwenye mifumo ya serikali yake ili waweze kuleta taaluma yao katika kuongeza ajira, huku wao wakiendelea na kazi sehemu zao za kazi. Kwa sasa wanataaluma hasa wa vyuo vikuu wameachwa nje ya mifumo rasmi na taaluma yao imekuwa frustrated kwakua wanatumiwa ndivyo sivyo katika kulisaidia taifa kujikwamua kiuchumi. Wengi wanaonekana kukata tamaa jambo ambalo nadhani Mh. Atafute jinsi ya kuwafikia siyo kupitia viongozi bali wao wenyewe kama alivyofanya Mh. Rais wa awamu ya tano kwa wafanya biashara na wachimba madini.
Nchi zote duniani viongozi wao wana fellowship ya ukweli na wanataaluma si kwakuwapeleka serikalini bali kuwaruhusu kuingiliana na utendaji wa serikali siyo kwakuchagua watu au group la watu bali kila mmoja kwa nafasi yake na taaluma yake na wakati mwingine kuachiwa kutengeneza hiyo mifumo na kuifanyia majaribio kuona kama ina match na uhalisia wa nchi yetu kwanza kabla ya serikali kui adopt na kuitumia katika uongozi wa shughuli zake.