Serikali itazame upya Sera za kuendesha uchumi na watu sahihi wa kuendesha uchumi

Sky Eclat

ndyo maana nasema,serikali kama iko serious,moja ipeleke miswada bungeni ya kubadilisha,kufuta au kutunga sheria rafiki za kodi,uwekezaji na mazingira rafiki ya biashara.

serikali iache kuvuna isipopanda.

huo mfano wako wa kiwanda cha mananasi ni kitendo cha serikali kula ugali ambapo hawakupeleka mboga.

serikali isiyobunifu huwaibia hata wananchi wake.
 
Peleka proposal yako ya kuanzisha kiwanda cha kukamua mananasi na usubiri kodi utakayoletewa kabla hata hujaanzisha biashara.
HIVI KILE KIWANDA CHA KUSINDIKA MANANASI KULE KIBAIGWA AMBACHO KIKWETE ALIWAAAHIDI WAKWERE WENZAKE AMGEKIJENGA ALIWAJENGEA?
 
Watunga sera ndio wanapaswa kulaumiwa kwa sababu wanalipwa mishahara kutunga sera bora kama hawawezi waondoke.
 
Reactions: Ame
Wizara ya fedha ilihitaji waziri msomi nguli wa uchumi na/au biashara aliyefanya kazi na kuwa uzoefu mkubwa katika sekta binafsi na pia aliyepata mafanikio makubwa katika sekta binafsi nchini.

Hii ni kwa sababu mawaziri karibia wote wa fedha ambao tumekuwa nao ni watu waliokulia katika utumishi wa umma na siasa, wanakosa weledi na fikra pana kuoona uchumi wetu kama kampuni ya kibiashara inayotakiwa kuzichangamkia fursa na kukua kila siku. Lugha kubwa wanayozungumza kila mara ni kodi na udhibiti.

Kama nchi lazima tupate watu wanaotambua kwamba kushamiri kwa biashara katika nchi ndio njia pekee ya kuumaliza umaskini wetu, watu waliokulia katika utumishi wa umma huwa hawana mindset hiyo kwa sababu kuendelea kuwepo kwao serikalini hakutegemei serikali kufanya vibaya au vizuri tofauti na wenzao katika sekta binafsi.

Mipango, sera, sheria,matamko n.k kama havifanikishi biashara tutaendelea kwenda mwendo wa kuchechemea katika maendeleo na tutakuwa tunaendelea kuwa na misafara ya viongozi kufungua viwanda vidogo vya kuajiri watu kumi ishirini na tutashangilia kama mafanikio makubwa. Tunapaswa tupate watu wanaowezesha zaidi biashara kufanyika badala ya kudhibiti tu.Tunapaswa kuwa na viwanda vikubwa vingi vinavyoajiri maelfu ya watu ili vijana waachane na boda boda na umachinga.
 
Reactions: Ame

Mambo yote yanaanzia Bungeni ,Bunge dhaifu la kina kibajaji na Mkuu NDUgai badala ya kuishauri serikali wao wanaikingia kifua.
 
Ataanza mama yako halafu utafuata wewe!

Kama MUNGU ni mjomba wako subiri utaona!

Mb*a wewe!
Meko kafa kaoza kibudu kabisa kabisa ananuka!
Alijikuta mungu mtu akafikiri hatakufa, sasa hivi kila siku usiku anachezea dushee la shetani, pole voicer, mume wako kaolewa huko jehanamu
 
Tuliambiwa idadi ya viwanda ambayo awamu ya tano imezalisha ni 2,400. Kama hili lingekuwa sahihi tatizo la ajira kwa vijana lingepungua.
Hebu fikiria, hiyo ni serikali inatangaza uongo ulio wazi kama huo, na wananchi wanaendelea kufurahi!
 
Watu wanaoweza kuupeleka uchumi mbele ni kama ifuatavyo.
1. Serikali inawahujumu na kuwasema ni wezi ili kabila maarufu sana Tanzania kwa sababu wanajua na iko kwenye damu Yao namna ya kuanzisha na kuendeleza biashara.
2. Serikali ingewachukua hili kabila na kulichanganya na makabila mengine ili wapate kitu kizuri. Mfano Bot: unamweka waziri ambaye hajawahi kufanya biashara hata ya kuuza pipi alivyokua mdogo. Ndio madhara yake wanasema watu wapeleke pesa benki. Hajui afanye nini
3. Ndio maana marekani hawa majews wameaachwa kwenye financial system na mambo Yao yanakwenda.
4. Serikali iunde sheria ya kunyonga. Hata kama mtu akiiba lazima anyongwe kama china. Lakini hakuna kuonea mtu. Angalia , maraisi wastaafu, mawaziri wastaafu na wengineo hawajanyongwa hadi leo. mnamuonea kingwa..
5. Kama mnaogopa kunyongwa. Kamata na fungia ndani na taifisha mali zote. Angalia mifano nchi za ulaya na marekani.
 
Yule Chizi alisema tuzaane kwa wingi,lakini ukweli ni tupunguze kuzaana bila michongo
 
Tusiizingizie elimu, swala la ajira limetengenezwa na mifumo ya dunia Kwa sababu maalumu Africa ikiwemo kuwatumia vijana ku destabilize serikali zitakazokaidi maelekezo yale ya jumla ya wenye nguvu za kiuchumi...

Hakuna shida ya kuajiri Tanzania na elimu hii ni sahihi kwakua duniani kote wasomi wa Tanzania wana fit wanapoendelea na masomo yao kwenye vyuo vingine nje ya nchi; ila imekosa sehemu ya kufanyiwa mazoezi ya ukweli ambayo ndiyo hiyo ajira na hivyo kuna mismatch kati ya matumizi ya rasilimali watu na kazi wazifanyazo, hivyo hao wasomi kushindwa kuwa mahiri katika nyanja zao. Hii inaongeza umasikini na pia kusababisha nchi kushindwa kujitegemea. Ikitokea hivyo tunaendelea kuwa tegemezi na nchi zetu zinaendelea kutotumia rasilimali zake inclusing watu, hivyo kuwawezesha hayo mataifa kuendelea kuzitumia kwaajili ya viwanda na matumizi yao mengine. Hii pia huwapa nafasi ya kuendelea kutawala masoko na kuendelea kuwa mataifa yenye nguvu duniani.

Pamoja na hayo yote, bado kuna sababu za msingi mataifa hayo kufanya hivyo na hata tukikubali kuwa kama wao watakavyo bado hali ingekuwa afadhali kama wachumi wetu wangeondoka katika kulazimisha model zile za darasani ambazo hazi fit vizuri kwenye nchi zetu kwasababu hizo hizo nilizotaja hapo juu kwakua uchumi wetu bado haujafikia kiwango cha soko i.e market economy ambapo sasa model hizo zingeweza kufaa.

Kilimo kwamfano, ni sehemu ambayo inaweza kuajiri vijana karibu wote wasomi wa Tanzania na kikizingatiwa katika context yake kingeweza bado kuelekeana na hiyo mifumo ya kiuchumi ya dunia pasipo misuguamo mikubwa na kwakutumia negotiation na diplomacy za kibiashara. Lakini nimesikitishwa kidogo juzi na maelezo ya Waziri wa kilimo kwamba wanadhamiria kununua piki piki kwa wagani ili wawatembelee wakulima...Japo bado ni mwanzoni, lakini naona failure kabla ya kufikia mwisho na kuona outcome. Hii ni kwakua mbinu hii imepitwa na wakati na ni mzigo mno kwa taifa ukiangalia pesa ambazo zitahitajika na kiwango cha uwezo wa mkulima huyo anayemlenga kumpa huduma hiyo kuongeza tija...We fikiria huyo mgani ambaye siyo sehemu ya uzalishaji wa moja kwa moja umlipe mshahara na marupu rupu yake, umwekee mafuta ya pikipiki akatembelee wakulima let say 30 au hamsini kwa siku atatumia muda gani kutoa elimu gani ambayo huyo mkulima pamoja na level yake ya elimu na vipingamizi vingi alivyonavyo including household labour ambayo wengi ndiyo hao wamekimbilia mijini na hawana ajira, kuongeza tija?

Hizo bilioni zitapotea jinsi ile ile hizo bilioni za mikopo kwa vijana na wanawake zinavyopotea kwakua zinasambazwa kwa watu wengi wasio na uwezo wa kuongeza tija.

Pesa hizo zikitumiwa kwa jinsi nyingine ambayo hapa siwezi kueleza kwasababu maalumu zitaweza kuajiri hao vijana wote waliosoma na wasio soma kisha wakaongeza tija na kutengeneza uchumi ulio imara na wenye uhakika wa soko la ndani...

Muundo ninaouwaza utawavuta vijana wa mjini kurudi vijijini kupata ajira na hiyo mikopo itafaa kuchochea uchumi tofauti na sasa ambapo unatumiwa kuwa madalali wa bidhaa za china, hivyo kutengeneza uchumi wa china zaidi kuliko ule ya Tanzania na Africa.

Mh. Mama Samia ni msikivu, mtulivu, kwa mara hii ninamatumaini atawasikiliza wataalamu wa Tanzania si kisiasa wala si kwakuwapa vyeo bali kuwa integrate kwenye mifumo ya serikali yake ili waweze kuleta taaluma yao katika kuongeza ajira, huku wao wakiendelea na kazi sehemu zao za kazi. Kwa sasa wanataaluma hasa wa vyuo vikuu wameachwa nje ya mifumo rasmi na taaluma yao imekuwa frustrated kwakua wanatumiwa ndivyo sivyo katika kulisaidia taifa kujikwamua kiuchumi. Wengi wanaonekana kukata tamaa jambo ambalo nadhani Mh. Atafute jinsi ya kuwafikia siyo kupitia viongozi bali wao wenyewe kama alivyofanya Mh. Rais wa awamu ya tano kwa wafanya biashara na wachimba madini.

Nchi zote duniani viongozi wao wana fellowship ya ukweli na wanataaluma si kwakuwapeleka serikalini bali kuwaruhusu kuingiliana na utendaji wa serikali siyo kwakuchagua watu au group la watu bali kila mmoja kwa nafasi yake na taaluma yake na wakati mwingine kuachiwa kutengeneza hiyo mifumo na kuifanyia majaribio kuona kama ina match na uhalisia wa nchi yetu kwanza kabla ya serikali kui adopt na kuitumia katika uongozi wa shughuli zake.
 
I concur...Mawaziri wetu wengi ni wanasiasa na wanakosa practical skills katika kuelewa what realy are the facts on the ground na hitaji lake ni lipi kama solution ili kuwe na tija endelevu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…