Serikali itenge magereza yenye kazi ngumu kwa wafungwa wanaorudia makosa wakiachiwa

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,900
Reaction score
52,056
Kuna wafungwa huona maisha ya gerezani raha sababu mengi hayana kazi ngumu.

Nashauri kwa wale watenda makosa ambao wakifungwa wakiachiwa wanarudia makosa wawe na magereza yao maalum yenye suluba za kazi za uhakika.

Hivi gereza la Maweni au magereza ya kupasua kokoto hayawezi wafaa? Serikali ifikirie hilo ili hawa warudia makosa wawekwe mahali pa kujua kuwa gereza sio hoteli.
 
We unafikiri wanapenda sana kukaa gerezani?

Sifurahii hiyo hali lakini kwa mtu ambaye alishapoteza dira ya maisha yake, alishapoteza mke na watoto alishapoteza kazi; ni ngumu sana kwake kujiandaa kisaikolojia kuhimili maisha ya duniani!

Ngoja siku wakusukumie huko ndani uone moto wake!
Umekaa kwenye kiyoyozi unakula machips unadhani dunia ni rahisi kwa watu wote?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ya kazi ngumu isubiri kwanza. Mie shauku na hamu yangu kubwa ni kuonavmahakama ya mafisadi ikifanya kazi na kutekeleza majukumu yake pasipo upendeleo.

Kila kukicha tunahubiriwa majukwaani kwamba kuna mafisadi na watu wametafuna hii nchi, mbona hiyo mahakama hatuoni ikiungurumisha hizo kesi?
 
Nikuambie jambo, binadam ni tofauti na mnyama nae mnyama huwezi kumlazimisha kulima/kubeba mzigo kama amechoka nakwambia utamuua bure kwa kipigo lakini haendelei na kazi.

Hapa gereza la Songwe Kuna mwaka mfungwa alimfyeka mguu nyapara sababu nyapara alikua akimchapa bakora mfungwa, mfungwa akaona kama ni noma na iwe noma.

Pale gereza la ruanda Mbeya askari magereza walimpiga jamaa nusu kuua lakini jamaa aligoma katu katu kwenda kulima.
 
Kuna wafungwa huona maisha ya gerezani raha sababu mengi hayana kazi ngumu.

Nashauri kwa wale watenda makosa ambao wakifungwa wakiachiwa wanarudia makosa wawe na magereza yao maalum yenye suluba za kazi za uhakika.

Hivi gereza la Maweni au magereza ya kupasua kokoto hayawezi wafaa? Serikali ifikirie hilo ili hawa warudia makosa wawekwe mahali pa kujua kuwa gereza sio hoteli.
Uko sahihi sana ndugu yangu. Mimi pia nashauri hivyo, na kuwe na condition mbili zifuatazo kwa wanaopta msamaha:

MOJA: Ukitoka kwa msamaha halafu ndani ya kipindi kisichozidi let's say miaka miwili au mitatu au kadhaaa...., ukawa umefanya kosa tena, ikitokea ukahukumiwa kifungo basi inabidi uende ukafungwe kwenye Gereza spesho kwa ajili ya kazi ngumu zaidi, tofauti na lile ambalo uliwahi kufungwa mwanzo

MBILI: Msamaha unapotoka, mfungwa asiyependa kutoka Gerezani, asilazimishwe kutoka Gerezani. Wafungwa wapewe hiari ya kuchagua wenyewe, aidha kutoka au kubaki pindi msamaha unapotoka. Isiwe ni lazima kwamba kila anayepata msamaha lazima atoke, maisha ni popote.

KUHUSU WAFUNGWA WANAOMALIZA MUDA WAO LAKINI WANAPENDA KUENDELEA KUBAKI GEREZANI, KAMA WAPO

Hawa nao waruhusiwe kubaki, na kama kutakuwepo lile Gereza spesho kwa ajili ya kazi ngunu, wapelekwe huko kwa sababu inaonyesha kuwa wanapendelea kuendelea kuishi katika mazingira ya kufanya kazi ngumu

Watu wa aina hii wanapotoka magerezani, wanaleta changamoto za ajabu sana uraiani. Bora wakaendelea kubaki huko kama wanapendelea wao wenyewe kubaki huko, ili mradi tu hawajashuurutishwa kuamua hivyo!
 
Maisha ni popote?
Wewe mbona hauendi jela?
Uko sahihi sana ndugu yangu. Mimi pia nashauri hivyo, na kuwe na condition mbili zifuatazo kwa wanaopta msamaha:

MOJA
: Ukitoka kwa msamaha halafu ndani ya kipindi kisichozidi let's say miaka miwili au mitatu au kadhaaa...., ukawa umefanya kosa tena, ikitokea ukahukumiwa kifungo basi inabidi uende ukafungwe kwenye Gereza spesho kwa ajili ya kazi ngumu zaidi, tofauti na lile ambalo uliwahi kufungwa mwanzo

MBILI: Msamaha unapotoka, mfungwa asiyependa kutoka Gerezani, asilazimishwe kutoka Gerezani. Wafungwa wapewe hiari ya kuchagua wenyewe, aidha kutoka au kubaki pindi msamaha unapotoka. Isiwe ni lazima kwamba kila anayepata msamaha lazima atoke, maisha ni popote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wafungwa huona maisha ya gerezani raha sababu mengi hayana kazi ngumu.

Nashauri kwa wale watenda makosa ambao wakifungwa wakiachiwa wanarudia makosa wawe na magereza yao maalum yenye suluba za kazi za uhakika.

Hivi gereza la Maweni au magereza ya kupasua kokoto hayawezi wafaa? Serikali ifikirie hilo ili hawa warudia makosa wawekwe mahali pa kujua kuwa gereza sio hoteli.

Hilo Gereza lilindwe kwa Mamba wenye Njaa kali au Simba!
 
Maisha ni popote?
Wewe mbona hauendi jela?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa na wewe fikiria vizuri! Mtu anataka kubaki jela, anatoka kwa shingo upande halafu anakuja anatafuta namana ya kufanya kosa ili arudi tena arudi jela. Matokeo yake anaamua kuja kuvamia nyumbani kwako anaiba na kukuacha umezimia, amekkupiga ngeo kichwani. Vipi kwa akili yako hiyo hali utaifurahia zaidi kuliko ile ya kumruhusu abaki gerezani kama hapendi kutoka?
 
We unafikiri wanapenda sana kukaa gerezani?

Sifurahii hiyo hali lakini kwa mtu ambaye alishapoteza dira ya maisha yake, alishapoteza mke na watoto alishapoteza kazi; ni ngumu sana kwake kujiandaa kisaikolojia kuhimili maisha ya duniani!

Ngoja siku wakusukumie huko ndani uone moto wake!
Umekaa kwenye kiyoyozi unakula machips unadhani dunia ni rahisi kwa watu wote?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nakuunga mkono.
Mtoa mada anaonekana Bado mtoto na Bado hajaijua dunia.
Anafikir akiwa innocent ndio hawezi kwenda jela hajui kuwa dunia ya Sasa imejaa fitina kila Kona.
Hajui kwamba hata sehem za ibada watu wanakwaruzana na kufikishana pabaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ya kazi ngumu isubiri kwanza. Mie shauku na hamu yangu kubwa ni kuonavmahakama ya mafisadi ikifanya kazi na kutekeleza majukumu yake pasipo upendeleo.

Kila kukicha tunahubiriwa majukwaani kwamba kuna mafisadi na watu wametafuna hii nchi, mbona hiyo mahakama hatuoni ikiungurumisha hizo kesi?
Hilo ndio Jambo la msingi sio kila siku magereza yanajaa wezi wa kuku tu waliosababishiwa na vyuma kukaza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao uwa wana matatizo ya kisaikolojia anashindwa aanze vipi maisha ya uraiani au KAACHA BASHA WAKE JELA.
wanapaswa kusaidiwa
Sasa na wewe fikiria vizuri! Mtu anataka kubaki jela, anatoka kwa shingo upande halafu anakuja anatafuta namana ya kufanya kosa ili arudi tena arudi jela. Matokeo yake anaamua kuja kuvamia nyumbani kwako anaiba na kukuacha umezimia, amekkupiga ngeo kichwani. Vipi kwa akili yako hiyo hali utaifurahia zaidi kuliko ile ya kumruhusu abaki gerezani kama hapendi kutoka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wafungwa wanatakiwa wasaidiwe kiakili....ubabe muda mwingine huwafanya wafungwa wawe sugu na kukata tamaa na maisha mengine, binadamu kuna wakati anahitaji faraja hata kama ni mkosaji... faraja na matumaini humrudisha kuwa mwerma.
 
We unafikiri wanapenda sana kukaa gerezani?

Sifurahii hiyo hali lakini kwa mtu ambaye alishapoteza dira ya maisha yake, alishapoteza mke na watoto alishapoteza kazi; ni ngumu sana kwake kujiandaa kisaikolojia kuhimili maisha ya duniani!

Ngoja siku wakusukumie huko ndani uone moto wake!
Umekaa kwenye kiyoyozi unakula machips unadhani dunia ni rahisi kwa watu wote?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ahahahahahaha jamaa anakula machips na ma broiler bhac anafikiri maisha yako sawa kwa watu wote ...kweli kaonyesha jinsi gan akili yake imeganda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom