Wakati sasa umefika kwa mamlaka husika kutoa bei elekezi kwa maji ya kunywa ya chupa! Pamoja na kutofautiana ubora wa vifungashio, naona dhuluma kubwa kwa mlaji ikizingatiwa maji safi na salama ni uhai na haki ya msingi kwa binadamu wote, na haki hii haina budi kutajwa kwenye rasimu ya katiba. Leo hii ukitoka nje ya mji kama unasafiri utauziwa maji ya kilimanjaro nusu lita sh.1,000/- na bei hiyo hiyo kwa maji ya uhai ya lita moja....Aibu...Aibu....Aibu!