#COVID19 Serikali itoe msimamo wake katika kupambana na corona

David M Mrope

Senior Member
Joined
Jul 13, 2021
Posts
115
Reaction score
74
Najua hii ni sehemu nyeti sana lakini hatunabudi kufahamishwa vizuri. Bado watanzania tupo katika mipasuko mikubwa mitatu. Sasa serikali inapaswa kuchukua hatua kabla huu ugonjwa haujashamiri vilivyo.

Serikali inayowajibu sasa kutueleza wananchi wapi tusimame katika kupambana na corona. Kwanza inawabidi wajue kuna makundi matatu ya watu,na haya yametokea baada tu ya serikali kubadilika. Makundi haya ni kama yafuatayo;

(i) WAPO WANAOAMINI CORONA INASHINDWA KWA DAWA ZA ASILI.
Hili ni kundi la kwanza. Kundi hili haliamini kabisa kuhusu wanasayansi. Kundi hili liliibuka kwa haraka sana maeneo ya vijijini. Hawa watu habari ya barakoa,chanjo & maombi hawayaamini kabisa.

Serikali inapaswa kujua hili kundi lipo. Na linaendelea kuwepo na litaendelea kuwepo mpaka pale serikali itapoamua kuusema ukweli wa ugonjwa huu.

(ii) WAPO WANAOAMINI CORONA INASHINDWA KWA MIUJIZA YA MUNGU.
Pia hapa Tanzania,hili kundi lipo. Wengi wao ni waumini wazuri wa dini. Kumbuka dini inaushawishi mkubwa katika jamii. Hivyo kundi hili ndio kundi kubwa zaidi ya kundi lolote. Wakati wote huamini Tanzania ni nchi teule.

Serikali bado inayo nafasi ya kutoa tamko juu ya kundi hili. Na inanafasi ya kuwaambia ukweli kabla ya hili gonjwa halijazidi.

(iii) WAPO WANAOAMINI CORONA INASHINDWA KWA NJIA ZA KISAYANSI.
Hili ni kundi dogo sana kwetu. Lakini kundi hili ndio kubwa zaidi duniani kote. Wengi huamini katika chanjo na njia zote za kisayansi na tunashuhudia nchi nyingi maambukizi yamepungua kwa kutumia njia hii.

Sasa hapa kwetu serikali ya awamu ya tano haikuamini katika chanjo,serikali ya awamu ya sita inaamini katika chanjo. Hapa watu wamechanganywa vyakutosha.

Saizi ukimfuata mtu huko kijijini ukamwambia vaa barakoa,hatokuelewa watu wameshachoshwa na taarifa kila kiongozi anasema lake. Jana kiongozi anasema tujifukize leo anakuja yuleyule na kusema tuchanjwe.

Hili jambo ni baya sana. Serikali ichukue hatua mapema ya kutuweka wote katika mtazamo mmoja na kuamua tunaenda wapi. Badae hali ikiwa mbaya itakuwa kazi kusikilizwa,kwani leo mnatuambia chanjo hiyari kwamba hata usipochanja hakuna madhara?

Kula lazima kuoga hiyari.
Serikali ituambie kipi chakula na yapi maji ya kuoga.

DAVID M MROPE.
SUA.
 
Kundi #3 hapo si wachache. Kundi hili lina wengi wa walioelimika. Kumbuka kuelimika si lazima kwenda shule.

Kundi #2 hilo ni dogo zaidi. Hao si taabu kwani wanawahi mbinguni.

Kundi #1 hao ni vyawa wa mwendazake. Hao wana matatizo ya elimu zaidi kuliko changanyika na kuwa brainwashed.

IMG_20210711_205649_038.jpg

Serikali wanaujua ukweli wote kuwa ugonjwa huu upo, unazidi kusambaa na kuzidi kuuwa watu. Wanajua ugonjwa huu unakwenda na kurudi mithili ya mawimbi.

Serikali hawana nia ya kupambana na ugonjwa huu maana wao tayari wameshaanza chanjo zilizo bora na wako salama:

IMG_20210718_063653_881.jpg

Kwa vile wao wako salama, basi kwao ugonjwa huu haupo.

Kungekuwa na nia ya kupambana na ugonjwa huu Wajaliwa na vigogo wote wa wizara ya afya waliokuwa awamu ya tano hawakupaswa ofisini sasa.

Huu ndiyo ulio ukweli mchungu.
 
Kundi #3 hapo si wachache. Kundi hili lina wengi wa walioelimika. Kumbuka kuelimika si lazima kwenda shule.

Kundi #2 hilo ni dogo zaidi. Hao si taabu kwani wanawahi mbinguni.

Kundi #1 hao ni vyawa wa mwendazake. Hao wana matatizo ya elimu zaidi kuliko changanyika na kuwa brainwashed.

View attachment 1859137

Serikali wanaujua ukweli wote kuwa ugonjwa huu upo, unazidi kusambaa na kuzidi kuuwa watu. Wanajua ugonjwa huu unakwenda na kurudi mithili ya mawimbi.

Serikali hawana nia ya kupambana na ugonjwa huu maana wao tayari wameshaanza chanjo zilizo bora na wako salama:

View attachment 1859138

Kwa vile wao wako salama, basi kwao ugonjwa huu haupo.

Kungekuwa na nia ya kupambana na ugonjwa huu Wajaliwa na vigogo wote wa wizara ya afya waliokuwa awamu ya tano hawakupaswa ofisini sasa.

Huu ndiyo ulio ukweli mchungu.
Dah nimejifunza kitu kutoka kwako.
 
Dah nimejifunza kitu kutoka kwako.

Panapo majaliwa vinjari huku pia:

Back
Top Bottom