Serikali itoe tamko la kulaani tabia mbaya

Serikali itoe tamko la kulaani tabia mbaya

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,340
Reaction score
4,659
Dunia inaendelea kupiga hatua za kimaendeleo ikichagizwa na ukuwaji wa sayansi na teknolojia, ukuwaji huu unaenda sambamba na kuongezeka kwa tabia au mfumo mbaya ambao unaenda kuvunja na kuharibu kabisa tamaduni za Afrika lakini pia hata sheria za dini tofauti.

Maendeleo haya ya teknolojia bado yanaenda kutuzalishia jamii isiyokuwa na maadili huku serikali bado haijatoa tamko rasmi licha ya kuwepo matukio mbalimbali ambayo yanadhihirisha athari za teknolojia katika jamii yetu.

Majuzi tulishuhudia jeshi la polisi likizalilishwa kupitia askari mmoja ambaye inasemekana kuwa ni muumini wa mapenzi ya jinsia moja watu wanaenda mbali zaidi wakidai kuwa vyama vya mashoga vinaweza kuwa na nguvu zaidi ya jeshi letu wakati kitu ambacho siyo sahihi.

Ukimya huu wa serikali kulaani vitendo vya mapenzi ya jinsia moja ni hafifu licho kuongezeka kwa idadi kubwa ya vijana hawa ambao nguvu kazi ya kesho kusema kweli sitarajii kuongozwa shoga katika maisha yangu hivyo tunaomba serikali iweze kujitathmini katika utekelezaji wake huku kulegalega kunaendelea kuitia doa jamii,dola na serikali yetu kwa ujumla.

Uhuru wa teknolojia usivuke mipaka na kuvunja tamaduni zetu, tamaduni ndiyo msingi mkubwa ambao unafanya mpaka sasa serikali iliyokuwepo madarakani kuendelea kuwepo hivyo basi ikiwa serikali itashindwa kusimamia jambo hili inatakiwa kutambua kuwa inapoteza nguvu/ushawishi kwa wananchi wake(sio wapiga kura nieleweke).

Zaidi: serikali inahitajika kuweza kusimamia vizuri hizi sheria za mtandao ili kupunguza au kutokomeza mambo ya konektion.
 
Naona mada za ushoga zinapewa kipaumbele sana na watu. Kataa ndoa mmataka muizime au sio🤬
 
Dunia inaendelea kupiga hatua za kimaendeleo ikichagizwa na ukuwaji wa sayansi na teknolojia,ukuwaji huu unaenda sambamba na kuongezeka kwa tabia au mfumo mbaya ambao unaenda kuvunja na kuharibu kabisa tamaduni za Afrika lakini pia hata sheria za dini tofauti...
Kemea na linda familia yako usisubiri serikali
 
Uhuru wa teknolojia usivuke mipaka na kuvunja tamaduni zetu
Hivi hadi leo bado unaamini ushoga umeletwa na teknolojia?

Mimi naona teknolojia ndio inasaidia kuibua na kutahmini hali ya hizi tabia kwenye jamii maana ni lahisi sana kujua tukio ata litokee wapi onspot unapata taarifa.
 
Kwa asilimia kubwa zaidi ya 70 ushoga unakuzwa na teknolojia.
 
Inamaanisha Mnapenda hayo matukio. Unaweza kuta hata ile video uliiangalia. Hebu kaushieni hizi mambo aisee
Hapana, ila tunakwenda but hatuna airtime hiyo wanaokuza ushoga ndiyo wanaopata jukwaa kubwa zaidi.
 
Tanzania ushoga bado sio tatizo wala kwanza sio wengi kiivo.ila kuna kahali ka kushabikia hizi topic sjui kametokea wapi.

Serikali haina haja ya tamko lolote katazo la ushoga lipo kisheria hivo itoe maagizo ya ndani kukagua material za kufundishia wanetu, kuzuia catoon, movies, miziki yenye mada za ushoga ikiwemo hata za kuupinga.

Kwa kifupi waunyime usagaji n'a ushoga airtime
 
Tamko au msimamo wa serikali kuhusu ushoga ni huu hapa.
Nauwasilisha.
JamiiForums-460527473.jpg
 
Dunia inaendelea kupiga hatua za kimaendeleo ikichagizwa na ukuwaji wa sayansi na teknolojia, ukuwaji huu unaenda sambamba na kuongezeka kwa tabia au mfumo mbaya ambao...
Serikali ianze na kukemea wizi wa Kura! Sio jambo jingine lolote.
 
HATA HIZI NYUZI NI ZA KUFUNGIA SASA IMEKUA KERO kwan moderators kina nani humu?
 
Back
Top Bottom