Serikali itoe tamko rasmi

NANGI NYANDA

Member
Joined
Jan 15, 2015
Posts
39
Reaction score
6
Hivi karibuni kumetokea sintofahamu kuhusu ajira za walimu kwa mwaka 2015! Sintofahamu hii inatokana na kauli za Kikwete pamaoja na waziri wake ndugu Zambi!

Zambi alitamka ajira za walimu wa arts hazitakuwa kwa mkupuo kwa kuwa walimu hawa wametosha kama Kikwete alivyosema!

Hata hivyo utata mwingine unaletwa na mwaka 2015! Wapo wanaosema ajira za mwaka huu zitakuwepo kwa kuwa bajet yake ni ile ya 2014/15 na wapo wanaosema kuanzia sasa hizo ajira hazitakuwepo!

Kwa kuwa ndani ya forum hii kuna mawaziri na imani yangu hata wa elimu yupo ninaomba alitolee ufafanuzi suala hili ili tunaozisubir ajira hizi tuwe na taarifa sahihi!
 
ngoja tumngoje aje... Ila tegemea kuwapata mawazir uswaz wanakuja na majibu positive na negative vuta subira !.
 
Acheni uongo ajira zipo pale pale tena ni 20/03/2015
 
mmmhhh mnasema mziki kimeo huku mnacheza"kutwa kutukana walimu kumbe ajira mnaziulizia ulizia tuacheni sie tusiojiweza na ualimu wetu"nyie subirini uafisa utumishi
 
Hivi serikali itatoa lini hizi ajira zetu jamani?
Daaah yaani watoe tu hizo ajira maana hali ni teteeeee
 
mmmhhh mnasema mziki kimeo huku mnacheza"kutwa kutukana walimu kumbe ajira mnaziulizia ulizia tuacheni sie tusiojiweza na ualimu wetu"nyie subirini uafisa utumishi

Kwa kweli wengine tuna shida na ualimu na ndio maana niliusomea na kwangu ni wito! Wazitoe tu ajira zetu
 
Kwa kweli wengine tuna shida na ualimu na ndio maana niliusomea na kwangu ni wito! Wazitoe tu ajira zetu
bora we umesema wengine kutwa kutuponda humu mi sionagi haya kusema mi ni mwl popote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…