Hivi majuzi wakati waziri wa fedha akiwasilisha bajeti kuu ya serikali bungeni alisema elimu ya kidato Cha tano na sita nayo itakuwa bila ada. Jambo hili ni jema na la kupongezwa lakini kuna kitu hakipo sawa.
Wakati serikali ikitangaza hili jambo wanafunzi wanaokwenda kuanza form five mwaka huu ndo walikuwa wanaenda kuripoti mashuleni. Bahati mbaya wakati inatangaza kuwa elimu itakuwa bila ada kwa kidato Cha tano na Cha sita hakuna barua kuhusu jambo hili Wala waraka mashuleni.
Mbaya zaidi serikali haijapeleka hata sent moja huko mashuleni kwa ajili ya kutekeleza jambo hili. Kitu ambacho kimeleta usumbufu kwa wakuu wa shule kwani baadhi ya wazazi wanawapeleka watoto wao kuripoti bila chochote kabisa kwa madai ya kuwa serikali imeshatangaza ni elimu bila malipo swali la kujiuliza hawa watoto watakula nini?
Kwa maoni yangu naiomba serikali iwe inatanguliza barua au nyaraka kabla ya tamko na wanapotamka fedha ziwe zimeshafika huko mashuleni. Sambamba na hilo Kwenye hili serikali iwe committed kuingiza fedha kwa wakati katika shule husika isije ikawa kama ilivyo sasa hivi huko shule za msingi na sekondari ambako fedha zinachelewa kila mwezi.
Mfano hadi leo hawajaingiziwa fedha ya elimu bila malipo ya mwezi June.-2022.Ninatumaini ombi langu litapokelewa.