Serikali itolee ufafanuzi iliposema elimu bila ada kwa kidato cha tano, Mbona bado walimu hawajapelekewa fedha wala barua kuhusu jambo hili?

Serikali itolee ufafanuzi iliposema elimu bila ada kwa kidato cha tano, Mbona bado walimu hawajapelekewa fedha wala barua kuhusu jambo hili?

F4B

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2022
Posts
336
Reaction score
429
Hivi majuzi wakati waziri wa fedha akiwasilisha bajeti kuu ya serikali bungeni alisema elimu ya kidato Cha tano na sita nayo itakuwa bila ada. Jambo hili ni jema na la kupongezwa lakini kuna kitu hakipo sawa.

Wakati serikali ikitangaza hili jambo wanafunzi wanaokwenda kuanza form five mwaka huu ndo walikuwa wanaenda kuripoti mashuleni. Bahati mbaya wakati inatangaza kuwa elimu itakuwa bila ada kwa kidato Cha tano na Cha sita hakuna barua kuhusu jambo hili Wala waraka mashuleni.

Mbaya zaidi serikali haijapeleka hata sent moja huko mashuleni kwa ajili ya kutekeleza jambo hili. Kitu ambacho kimeleta usumbufu kwa wakuu wa shule kwani baadhi ya wazazi wanawapeleka watoto wao kuripoti bila chochote kabisa kwa madai ya kuwa serikali imeshatangaza ni elimu bila malipo swali la kujiuliza hawa watoto watakula nini?

Kwa maoni yangu naiomba serikali iwe inatanguliza barua au nyaraka kabla ya tamko na wanapotamka fedha ziwe zimeshafika huko mashuleni. Sambamba na hilo Kwenye hili serikali iwe committed kuingiza fedha kwa wakati katika shule husika isije ikawa kama ilivyo sasa hivi huko shule za msingi na sekondari ambako fedha zinachelewa kila mwezi.

Mfano hadi leo hawajaingiziwa fedha ya elimu bila malipo ya mwezi June.-2022.Ninatumaini ombi langu litapokelewa.
 
Yale ni mapendekezo ya kwenye bajeti mpya ya mwaka 2022/2023 ambayo bado hayajapitishwa rasmi kuanza kutumika, na kama yakipitishwa yataanza kutumika kwenye mwaka mpya wa Fedha kiserikali ambao huanza mwezi wa 7. Bajeti yapendekeza Elimu ya kidato cha tano na sita kutolewa bure

Hivyo kwa sasa bado tunatumia bajeti ya zamani ambayo haina kipengele cha elimu bila ada kwa kidato cha tano. Kwa hiyo wanatakiwa kuwapeleka watoto na ada mpaka itakapotekelezwa bajeti mpya.
 
Hayo ni mapendekezo tu kwa bajeti ya serikali mwaka wa fedha 2022/2023 bunge bado linajadili likipitisha utekelezaji wake ni kuanzia Julai 2022.
 
Sielewi kama nimeeleweka vizuri ? nimesema serikali iwe inatoa kwanza waraka Kisha tamako, ili kupunguza usumbufu usio kuwa wa lazima kwa wakuu wa wakuu au itoe ufafanuzi kwani kwani kwa sasa Kuna baadhi ya wazazi wanapeleka watoto wao kuripoti pasipo fedha yeyote wakidai serikali imeshasema elimu ya kidato cha tano na sita ni bure swali la kujiuliza watakula nini? hao watoto kabla ya kufikia July mosi ni hayo tu
 
Hayo ni mapendekezo tu kwa bajeti ya serikali mwaka wa fedha 2022/2023 bunge bado linajadili likipitisha utekelezaji wake ni kuanzia Julai 2022.
Ndo maana nikasema serikali itolee ufafanuzi ili jamii ielewe jambo hili
 
Sawa hili wamelipokea tuwe wenye subira kusubiria utekelezaji.
Wakati wanasubiri utekelezaji shule zitakuwa zinajiendeshaje? Mkuu kuendesha shule si mchezo hasa za bweni jamaa kaleta hoja makini sana. Nadhani wakati serikali inajiandaa kufanya utekelezaji wangeacha utaratibu wa zamani uendelee kwa wanafunzi wa mwaka huu wakati wakiweka mambo sawa. Then msimu ujao ndo utaratibu mpya uanze.

Huku kukurupuka kutawaumiza wanafunzi wenyewe.
 
Watanzania wanavyopenda dezo. Kuna wazazi hata hela ya viatu na nauli hawaandai wanawaambia watato wao serikali itawalipia
 
Mathalani imeshasema Elimu Bure A level basi tuondoe shaka naamini Hadi wameamua kutangaza hivyo inamaana ni uhakika chamsingi Tuupe muda nafasi yake na ikitokea ndani ya mwaka mmoja wananchi wakawa wanalipa michango basi tutawahoji.

Pongezi kwa Serikali kutoa Elimu Bure, ila isiishie tuu kupeka Feza kwa ajili ya Elimu bari ifanye jitihada za kuiboresha Elimu, isiwe Bure basi na huduma ikawa Bure kabisa, tunaamini walimu Kuna vimiradi mlianzisha hivyo kupitia hii Elimu Bure msikwazike na mkaanza kufanya Bora liende tuu hapana hii nchi yetu sote mkiwasaidia watoto wetu basi mmewasaidia watoto wenu kikubwa tusaidiane, msilete chuki kwa hili haya ni moja ya maendeleo kwa Taifa linalokuwa kiuchumi.
 
Watu wagumu kuelewa duniani huwa ni walimu.
Nina wasiwasi na elimu yako, bila walimu Leo usingejua hata kuandika huo utumbo wako, shame on you rubish! Unapata wapi haki ya kuwatukana walimu, mtoa mada kafafanua vizuri kuwa jamii ipewe ufafanuzi/ elimu kwani wanapeleka watoto bila Ada, sa usichoelewa hapo kitu gani?
 
Hivi majuzi wakati waziri wa fedha akiwasilisha bajeti kuu ya serikali bungeni alisema elimu ya kidato Cha tano na sita nayo itakuwa bila ada. Jambo hili ni jema na la kupongezwa lakini kuna kitu hakipo sawa.

Wakati serikali ikitangaza hili jambo wanafunzi wanaokwenda kuanza form five mwaka huu ndo walikuwa wanaenda kuripoti mashuleni.Bahati mbaya wakati inatangaza kuwa elimu itakuwa bila ada kwa kidato Cha tano na Cha sita hakuna barua kuhusu jambo hili Wala waraka mashuleni.

Mbaya zaidi serikali haijapeleka hata sent moja huko mashuleni kwa ajili ya kutekeleza jambo hili. Kitu ambacho kimeleta usumbufu kwa wakuu wa shule kwani baadhi ya wazazi wanawapeleka watoto wao kuripoti bila chochote kabisa kwa madai ya kuwa serikali imeshatangaza ni elimu bila malipo swali la kujiuliza hawa watoto watakula nini?

Kwa maoni yangu naiomba serikali iwe inatanguliza barua au nyaraka kabla ya tamko na wanapotamka fedha ziwe zimeshafika huko mashuleni. Sambamba na hilo Kwenye hili serikali iwe committed kuingiza fedha kwa wakati katika shule husika isije ikawa kama ilivyo sasa hivi huko shule za msingi na sekondari ambako fedha zinachelewa kila mwezi.

Mfano hadi leo hawajaingiziwa fedha ya elimu bila malipo ya mwezi June.-2022.Ninatumaini ombi langu litapokelewa.
Acha ujuaji, utekelezaji wa agizo hilo unaanza mwaka ujao hivyo wanaodaiwa hivi sasa wanatakakiwa walipe.
 
Wazazi karibia wote waliowapeleka watoto kidato cha tano wamelipia Ada, so sijui mto mada unataka nini kwenye huo mgao wa serikali..?
 
Wazazi karibia wote waliowapeleka watoto kidato cha tano wamelipia Ada, so sijui mto mada unataka nini kwenye huo mgao wa serikaha ha ha ha wanalipa ila baada ya maelezo marefu
 
Hivi mnajua bajeti ya serikali inafanyaje kazi? Bajeti huletwa, ikajadiliwa, ikapitishwa then inatunguliwa sheria ya kuruhusu matumizi yafanyike. Haya yote ni hatua ya kwanza sasa wapo kwenye hatua y da kujadili. Subirini hapo ndo ikipitishwa uulize hilo swali lako.
 
Back
Top Bottom