Serikali itufafanulie "hatua za mwisho" maana yake nini badala ya kutufanya kama watoto wadogo wa kudanganywa kwa majibu ya rejareja

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Mwaka jana, June 2023, wakati waziri wa mambo ya nje akiwa Dr Tax, serikali ilitoa hili tamko pale Bungeni

Leo April 2024, serikali imetoa tena tamko hilo hilo pale pale Bungeni mbunge wa viti maalumu Suma Fyandomo alipouliza swali kuhusu uraia pacha.

Sasa nakumbuka tumekuwa na matamko kama haya toka serikalini kuhusu SGR, umeme, bei ya sukari, huduma mbovu za polisi, huduma mbovu za maji, barabara mbovu, huduma za ATCL, nk.

Najiuliza, hivi tatizo ni sisi Watanzania, viongozi wetu, Bunge au Raisi Samia? Kwa nini tunadanganywa na serikali kama watoto wadogo kila siku juu ya mambo ya kila namna?

Kwamba tunadharauliwa kiasi hiki na viongozi wetu na wanatuona hatuna akili ya kukumbuka au kutafakari?

Tatizo letu liko wapi? Kwa nini tunakuwa watu wa namna hii?

 
"Black people are not complete human beings because they don't have a good brain to govern the society as White people. They are still under the process of becoming the complete human beings."
Pieter W. Botha, a former President of South Africa during the Apartheid era
 
Ulikuwa hujui mkuu?
Watanzania tumekuwa wajinga mno. Inafikia waziri mwenye daraka la kuangalia uchumi wa nchi anasema uchumi wa Tanzania umekua kwa sababu magari ya namba za "E" barabarani ni mengi, na bado tunakenua meno tu kumshangilia. Halafu anasema ana first class ya uchumi pale UDSM! Yaani tuanongozwa na watu wengine ni majuha kabisa, au wao wanatuona sisi majuha kabisa.

Mbaya zaidi, huyu mtu anataka aje kuwa Raisi wa Tanzania - shocking!!!
 
Yaani kaa utulie, ungojee mpaka uzeeke kuliko Mamndenyi
Kuna mapinduzi yalifanyika katika nchi za Afrika, na wale waliokuwa viongozi, mawaziri nk katika nchi hizo, walipelekwa uwanjani na kupigwa risasi hadharani. Tayari kichwani mwangu kuna list ya watu ambao ingekuwa Tanzania hilo linafanyika viongozi wepi wangestahili kufanyiwa hivyo
 
Black people are not complete because they allow situations whereby stupid people choose stupid people to be their leaders, while intelligent people just sit and watch from a distance, because they cant stand interacting with stupid people
 
Hilo suala la Uraia pacha liachwe kwanza Kwa Sasa, lisipoendewa vizuri matokeo yake yanaweza kuwa mabaya mbeleni
 
Ta
Tangu lini serikali ya CCM ikatoa ahadi ya kweli?
 
Hilo suala la Uraia pacha liachwe kwanza Kwa Sasa, lisipoendewa vizuri matokeo yake yanaweza kuwa mabaya mbeleni
Hiyo ni argument ambayo mimi binafisi siwezi kuikubali. Ilikuwa ni argument ya watu wenye mentality ya Magufuli na genge lake.

Kuna usemi kwamba "you dont have to reinvent the wheel"

Hadi sasa kwa miaka zaidi ya 10 iliyopita, 74% ya nchi duniani zimeruhusu uraia pacha. Kwa hapa Afrika Tanzania ni mojawapo kati ya nchi kama 11 kati ya 54 za Afrika ambazo bado haziruhusu uraia pacha.

Swali la kujiuliza, kwa nini issue ya uraia pacha itakuja kuwa tatizo kw Tanzania na haijawahi kuwa tatizo kwa nchi zinazouruhusu? Sisi tuna tofauti gani na nchi kama Rwanda ya Kagame, Kenya ya Rutto, nk, ambazo zilisharuhusu uraia pacha miaka kadhaa iliyopita na wala hatujasikia tatizo lolote kwao?

Na kumbuka pia, suala la uraia pacha lilipitishwa Bungeni, na Kikwete alipotakiwa kutia sahihi sheria ya uraia pacha akashauri kwamba badala ya kuipitisha in isolation ni vema iwekwe ndani ya katiba mpya. Sasa hapo ndio wale watu wenye ujima wakapata nafasi ya kuuanza kupinga bila hata kuelewa nini maana ya uraia pacha, na ni nani anapewa uraia pacha.

Bila Kikwete kutoa ushauri wa uraia pacha kuwa kwenye katiba mpya leo hii tungekuwa na uraia pacha. Kikwete alifanya kosa kubwa sana kutotia sahihi mswaada wa uraia pacha, japo alifanya kwa nia nzuri.

Halafu namshangaa sana Samia. Wazanzibar wengi watafaidika na uraia pacha kuliko watu wa bara, na wangeibadilisha Zanzibar. Samia ndio mwenye wajomba wa kumpa uraia huko uarabuni, sisi huku bara hatuna wajomba huko Oman au Dubai.
 
Hilo suala la Uraia pacha liachwe kwanza Kwa Sasa, lisipoendewa vizuri matokeo yake yanaweza kuwa mabaya mbeleni
Tatizo ni kwamba suala la uraia pacha Tanzania linajadiliwa na watu ambao hawaelewi maana ya uraia pacha, na hata 90% ya wabunge wetu hawajui maana ya uraia pacha na unatolewa kwa misingi gani. Angalia hizi thread hapa chini



Wengi wanaopinga uraia pacha, wanajua hawana nafasi ya kuja kuwa raia pacha

Wengi Wanaopinga Uraia Pacha Hawana Sababu za Msingi Kuupinga Kwa Sababu Hizi

 
Wa kwanza angekuwa Mwigulu.
 
Wa kwanza angekuwa Mwigulu.
Kama umenisoma kichwani!

Wa pili mtuhumiwa wa kuwanyima watu haki ya kuishi, kisha Mtu wa miundo mbinu, halafu ningeenda kwa IGPs na ma RPCs, wastaafu na waliopo...ni wengi mno!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…